Serikali ya Tanzania imetenga kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa nchini ili kuwawezesha wanafunzi hao kupata huduma ya elimu kama wanavyopatiwa watoto wengine.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya ufundi Moshi , walimu pamoja na maafisa elimu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwl. Julius K. Neystory amesma lengo ni kuhakikisha kuwa huduma ya elimu inawafikia watoto wote bila ubaguzi .
Mwl. Neystory amefafanua kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kununua vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili kukidhi changamoto wanazokabiliana nazo wanapokuwa shuleni ambapo shule ya sekondari ya ufundi moshi ni miongoni mwa shule zinazonufaika na fedha hizo.
Aidha Mwl. Neystory alipozungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari Mawenzi na Shule ya Sekondari Moshi Ufundi kwa nyakati tofauti amebainisha kuwa Serikali imedhamiria kurudisha heshima ya viwango vya elimu hapa nchini kwa kuendelea kuzikarabati shule zote kongwe ili kuleta tija ya ufaulu na kukuza kiwango cha elimu .
Mbali na hayo Mwl. Neystory amesisitiza umuhimu wa nidhamu kwa wanafunzi na kukumbusha kuwa ni chanzo cha mafaniko ya mwanafunzi katika elim; hivyo basi aliwaasa wanafunzi kutumia vizuri fursa ya miundombinu iliyokarabatiwa ili waweze kujifunza kwa usahihi na hatimaye kufaulu mitihani yao.
Mkurugenzi Neystory alifanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Kilimanjaro na kutembelea shule ya sekondari ya ufundi moshi na shule ya sekondari mawenzi ambazo ni miongoni mwa shule kongwe zilizoletewa fedha za ukarabati katika mkoa wa Kilimanjaro.
Katika ziara hiyo alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa shule za sekondari moshi ufundi na sekondari ya mawenzi na kuwataka kutumia muda wa masomo vizuri ili kuleta tija ya ufaulu itakayopeleka kuboresha maisha yao ya baadaye na kuimarisha uchumi wa nchi.
.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa