Watumishi wa umma katika wilaya Siha wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria kanuni, taratibu na mipaka ya kazi ya kila mmoja wao.
Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2019 Bwana Mzeee Mkongea Ali wakati wa kuagana na wananchi wa wilaya siha baada ya kukamilika kwa mbio za mwenge wa uhuru wilayani humo.
Ali a meongeza kuwa watumishi wanatakiwa kuwasilisha malalamiko na mataizo yao kwa waajiri au wakuu wao wa kazi kwa uwazi ili yatatuliwe kwa mijibu wa kanuni za utumishi wa umma badala ya kutumia mitandao ya kijamii kama majukwaa ya kutolea malalmiko yao.
Aidha kiongozi huyo amewataka viongozi na wananchi wote wa wilaya ya siha kufanya kazi kwa maelewano, upendo na ushirikiano ili lengo la serikali kuwawezesha wananchi kujiletea maendeleo litimie.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa