Watumishi wa umma katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kutumia kwa usahihi huduma na vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambavyo ni mali ya serikali.
Akiongea baada ya mafunzo ya matumizi sahihi ya TEHAMA kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimaliwatu Bw. Bwai Biseko amewataka watumishi hao kuzingatia mafunzo na maelekezo juu matumizi ya vifaa na huduma hizo kwa mujibu wa miongozo ya serikali.
Aidha Biteko amewataka watumishi waliohudhuria mafunzo kuwaelimisha watumishi wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo ili kuhakikisha kuwa watumishi wote wanafahamu na kuzingati maelekezo na miongozo ya matumizi ya TEHAMA serikalini.
Mbali na maelekezo hayo Biseko ameahidi kushiriana kwa karibu na Afisa TEHAMA na Afisa Habari wa wa Ofisi hiyo ili kuhakikisha kuwa matumizi sahihi ya TEHAMA yanazingatiwa sambamba na kutoa taarifa kwa wananchi kwa kupitia TEHAMA.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa