Seriakali imesitishisha mkataba wake na mkandarasi anayejenga mradi wa maji wa Same, Mwanga Korogwe katika chanzo cha maji bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani mwanga.
Akitoa tamko la serikali baada ya kutembelea mradi huo, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema serikali imefanya uamuzi huo baada ya mkandarasi A.M Kharafi & Sons aliyepewa kazi ya kujenga miondombinu ya maji kwenye chanzo kuchelewesha mradi huo huku wananchi wakiendelea kupata tabu ya kukosa huduma muhimu ya maji.
Mhe. Aweso kwa niaba ya serikali amewaomba radhi wananchi wanapata shida ya maji kutokana na kuchelewa kwa kukamilika kwa mradi huo.
Aidha Mhe. Aweso amemuagiza mkandarasi A.M Kharafi & Sons ahakikishe kuwa wananchi wote walifanya kazi katika mraadi huo wanalipwa stahiki zao zote wanazodai na serikali itasimamia kwa karibu kuhakikisha wananchi hao wanapata haki zao.
Mbali na hayo Mhe. Aweso amemtaka mkandarasi Badr East Africa Enterprises Ltd anayesambaza miuondombinu ya maji ikiwemo mabomba kuongeza kasi ya utekelezaji ili ifikapo mwezi Machi 2021 awe amekamilisha kazi kama mkataba ulivyosainiwa kwani serikalia haitatoa muda wa ziada endapo muda huo utafika bila kazi kukamilika.
Mradi wa maji wa Same Mwanga Korogwe unatarajiwa 438,000 wa wilaya za Mwanga, Same na Korogwe
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa