ZAHANAT YA KIMASHUKU
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Bw. Godfrey Mnzava ameweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Kimashuku leo Aprili 3,2024 na kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Hai pamoja na timu nzima kwa usimimazi mzuri wa mradi huo.
Aidha, Bw. Mnzava ameelekeza manunuzi yote yafanyike katika mfumo wa NesT na kuwajengea uwezo kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na watendaji na wasimamizi wote wanaotoa huduma za afya.
Akisoma taarifa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mganga mfawidhi wa wilaya ya Hai amesema mradi utaghatimu kiasi cha Tshs. Dkt. Itikija Msuya Milioni 117,500,000.00 hadi kukamilika kwa sasa umetumia kiasi cha Tshs. Milioni 76,214,168.00 na umetoa ajira kwa wananchi zipatazo 40 ikiwa wanawake 17 na wanaume 23.
Dkt. Msuya amesema mradi huu uliibuliwa na wanakijiji mwaka 2022 kwa lengo la kusogeza huduma za afya karibu ikiwa na lengo la kupumguza vifo vya mama na mtoto.
Zahanati hii inatarajiwa kihudumia wananchi 5,367 na kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje, klinik ya baba, mama na mtoto pamoja na chanjo.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa