• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kilimanjaro Region
Kilimanjaro Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kilimanjaro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia ya Mkoa
    • Viongozi wa Mkoa
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Sekretariati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Teknologia ya Habari na Mawasiliano
      • Internal Audit
      • Kitengo cha Sheria
      • Procument and Supply
    • Miongozo
  • Wilaya
    • Hai
    • Moshi
    • Mwanga
    • Same
    • Rombo
    • Siha
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hai
    • Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
    • Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Same
    • Halmashauri ya Wilaya ya Siha
    • Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Albam
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utekelezaji TASAF Kilimanjo Wamfurahisha Kapt. Mkuchika

Posted on: August 29th, 2018

Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Kapt(Mst.) George H. Mkuchika amesma ameridhishwa na utendaji wa viongozi na watumishi waratibu wa Tasaf  mkoani Kilimanjaro katika kusimamia utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf..

Mhe. Mkuchika amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi na viongozi wa  mtaa wa Msaranga kata ya Msaranga Manispaa ya Moshi.

Waziri Mkuchika amesema amefanya ziara ya siku tatu katika mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kujionea utekelezaji wa mpango huo ambao unasimamiwa na wizara yake na amejionea jinsi walengwa walivyonufaishwa na mpango huo na kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanufaika hao.

Amefafanua kuwa lengo la mradi wa Tasaf awamu ya tatu ni kuwasaidia wananchi wenye hali duni za maisha ili waweze kupata mahitaji muhimu ambayo ni  chakula, mavazi na malazi lakini katika mkoa wa Kilimanjaro manufaa ya mradi huo yamenda mbali zaidi na kuwanufaisha walengwa katika nyanja zingine za maisha.

"Mimi nimefurahi sana Tasaf katika mkoa wa kilimanjaro imewezesha watoto wa walengwa kuhudhuria kiliniki, kuhudhuria shuleni wakiwa na mahitaji muhimu ikiwemo sare na viatu na familia zao kuwa na bima za afya." Amesema Waziri Mkuchika.

Aidha baadhi ya walengwa waliopata fursa ya kuzungumza na Mhe. Mkuchika wametoa shukrani zao kwa serikali kwa kuwajali na kutambua uwepo wao.

Kwa nyakati tofauti mlengwa hao wakiwemo Bibi Tedy Lyatuu na Bibi Jelenais Ngowi wamemuomba Mhe. Mkuchika awafikishie salamu zao za shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.




Matangazo

  • Kwa Huduma Bora ya Ukumbi wa kisasa wa Mikutano, Tafadhali fika Ofisini au wasiliana nasi kwa S.L. P 3070, Moshi. au Piga simu namba 027 2758248/027 2751 February 03, 2020
  • Angalia Zote

Habari

  • MAHINDI YA TANZANIA NI SALAMA

    April 01, 2021
  • Viongozi Watakiwa Kusimamia Kilimo cha Kisasa

    March 05, 2021
  • Waziri Aweso Avunja Mkataba na Mkandarasi wa Mradi Mkubwa wa Maji

    December 25, 2020
  • Serikali Yarudisha Mali za Ushirika

    November 12, 2020
  • Angalia Zote

Video

Tamasha la Upimaji VVU Mkoa wa Kilimanjaro
Video

Kiunganishi cha Haraka

  • Webmail
  • Malalamiko
  • Fomu ya Opras

Tovuti zinazohusiana nasi

  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi (LIVE)
  • Manispaa ya Moshi
  • Mfumo wa Usambazaji Mafaili kwa njia ya Ki-Eletroniki (E-Office)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    Florida Street

    Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi

    Simu: 027 2758248/027 2751

    Mobile:

    Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa