Zaidi ya wananchi 7,000 kutoka vijiji sita vikiwemo Gararagua na Kideco wilayani Siha wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama kupitia mradi mkubwa wa skimu ya maji Lewate - Fuka, unaogharimu shilingi bilioni 2.03.
Awali, wakazi wa maeneo hayo walilazimika kutembea zaidi ya kilomita 7 kufuata huduma ya maji, jambo ambalo liliathiri shughuli zao za kiuchumi na kijamii, hususan kwa wanawake na watoto.
Akizindua rasmi mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Ismail Ussi, amepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kutekeleza ahadi zake, na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za msingi, ikiwemo maji.
Ndg. Ussi ameutaka uongozi wa wilaya ya Siha pamoja na wananchi kwa ujumla kulinda na kuhifadhi miundombinu ya mradi huo ili iwe endelevu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Aidha Mradi wa Gararagua - Kideco
ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa kupitia fedha za mfuko wa Maji wa Taifa (NWF) pamoja na fedha za malipo kwa matokeo (PforR) ambapo mradi huo umetoa ajira za muda kwa watu 158, ikiwa Wanaume 152 na Wanawake 6 wakiwa ni wakazi wa vijiji vya Sanya Juu, Merali,Ngumbaru, Naibili, Ngaritati na Loiwang.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa