Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Kiseo Nzowa amesema katika juhudi za boresha huduma ya usafiri na usafirishaji Mkoani Kilimanjaro Serikali imehakikisha ifikapo APRILI, 2026 kituo cha mabasi cha kimataifa cha Moshi (NGANGAMFUMUNI) kinaanza kutoka huduma za usafiri Kwa Wananchi wa Moshi.
Amesema hayo Agosti, 27,2025 katika hafla ya kumkabidhi Site Mkandarasi Mkuu CRJE (EAST AFRICA) LTD wa Dar es Salaam
Bw. Nzowa amesema mradi huu utakapoanza kutoka huduma utaongeza Ajira Kwa wakazi wa Moshi watakaofanya biashara katika STENDI hiyo na wale watakao ajiriwa nafasi mbalimbali pia itaongeza mapato katika Manispaa ya Moshi na Nchi Kwa jumla.
Hata hvyo, Bw. Nzowa ametoa wito Kwa Wananchi wa Moshi kuwa walinzi wa rasilimali zinazoletwa katika mradi huo wakati wa utekelezaji
"Kuna baadhi ya watu sio waaminifu, wanatabia ya kuchukua na kuuza vifaa vya ujenzi hvyo kila Mmoja wetu awe mlinzi wa mwenzake na kutoka taarifa katika vvyombo vya usalama.
Aidha, Nzowa amemtaka Mkandarasi na TIMU yake kuhakikisha mradi unakamilika Kwa wakati na Kwa viwango bora ili uanze kutoa huduma Kwa muda uliopangwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Godfrey Mnzava amesema halmashauri imekua kwenye mikakati mbalimbali ya kujenga vyanzo vipya vya mapato lengo ni kuweza kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Kwa upande Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe amesema ujenzi WA awamu ya Kwanza ambao umefikia asilimia 51 ya utekelezaji wake unagharimu kiasi cha shilingi 19,834,027,619,08 huku ukihusisha ujenzi WA jengo la abiria lenye gorofa mbili ambalo litakua na maduka,sehemu za kukatia tiketi,migahawa,maeneo ya kusubiria wakati wa kupakia au kushusha abiria eneo la kuhifadhia mizigo,vyumba vya Ofisi,vyumba vya idara ya uhamiaji,kituo cha polis,eneo la kupakia magari na tank la ujazo WA Lita 476,000 .
Aidha, amesema halmashauri imepokea shilingi bilioni 7,485,504,635.70 kutoka serikali kuu huku halmashauri ikichangia shilingi bilioni 1,248,746,423.54 na kufanya jumla ya fedha kuwa Shilingi 8,734,251,059.24.
Mwajuma amesema katika awamu ya pili ujenzi utahusisha jengo la hoteli lenye gorofa nne ambalo litakua na vyumba 48 vya kulala, mgahawa, supermarket,maduka, eneo la benki na sakafu ya chini ya kupakia magari madogo na daraja ambalo litaunganisha jengo la abiria na hotel ambalo chini mabasi yatapita na juu kutakua na maduka huku vikigharimu kiasi cha shilingi 9,030,621,703.77 hadi kukamilika.
Mradi huu ulianza rasmi tarehe 28/1/2019 na ulipaswa kukamilika tarehe 28/1/2021 kutokana na changamoto mbalimbali mkandarasi aliongozewa muda WA utekelezaji na kutarajiwa kukamilika rasmi APRILI,2026.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa