Wanachi wa wilaya Moshi wametakiwa kuendelea kutunza mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanajaro KINAPAili iendelee kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.
Akiongea na wanachi wa vijiji vya Kitowo na Kiraracha Kata ya Marangu Magharibi wilayani Moshi baada ya kukabidhiwa mradi wa zahanati katika kijiji cha Kitowo uliojengwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya Mlima na Kilimajaro KINAPA katika kijiji cha Kitole Mkuu wa wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba amewataka wananchi kutokuwa wabinafsi kwa kutumia rasilimali zilizopo katika hali ya kuziharibu na kuziangamiza jambo ambalo si sahihi hata mbele za mungu.
Mhe. Warioba amesema si fikra sahihi kwamba binadamu wulio karibu na rasilimali hizi kwa sasa wana haki ya kutumia hovyo bila utaratibu, hivyo basi rasilimali zote za hifadhi zitumike vizuri na wakati huohuo zitunzwe na ziongezwe ili ziwe endelevu. "Matumizi lazima yawe endelevu, watoto wetu hawa wana haki ya kunufaika na rasilimali hizi, hivyo basi tusidhani kwamba tunaruhusiwa kuvuna miti na wanyama wote ndani ya hifadhi hapana" Alisema Mhe. warioba.
Mbali na hilo Mhe Warioba amewakumbusha wananchi hao kuwa maji safi yanayotiririka kutoka kwenye hifadhi ya KINAPA yananufaisha wananchi wengi katika mikoa mitano kwa matumizi ya moja kwa moja ya majumbani na kiasi kingine cha maji kinaingia kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu linalozalisha umeme.
Aidha Mhe. Warioba amewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa hususan katika mwaka huu wa uchaguzi ili wasije kulaghaiwa kwa kuombwa kura kwa kuahidiwa kuwa wataruhusiwa kuingia ndani ya hifadhi bila kufuata sheria na tararibu.
Mhe Warioba amewataka wananchi wawe tayari kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu waharibifu wa mazingira na majangiri ili hatua za kudhibiti zichukuliwe mara moaja.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Dkt.Alex Kazula ameishukuru KINAPA kwani mradi huo unaongeza idadi ya vituo vya na kufanya vifikie 96 katika wilaya ya Moshi.
Dkt. Kazula ameongeza kuwa mradi huo unatarajiwa kuanza kutoa huduma tarehe moja mwezi machi mwaka hu, kwani hadi sasa tayari halmashauri imeshapokea jengo na samani, vinasubiriwa sasa ni vifaa tiba
Aidha Dkt. Kazula ameshukuru wizara ya Afya kwa kutoa kubali cha kuendesha kituo hicho hali kadhalika ameishukuru Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kutoa ruhusa ya kufungua akaunti ya kituo ili huduma zianze kutolewa.
Mradi huo ambao ni kutuo pekee cha serikali unatarajia kunufaisha zaidi ya wananchi 15,000 kutoka kwenye vijiji 6 vilivyomo katika kata ya Marangu Magharibi.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Kamishna Mwanadamizi wa TANAPA kanda ya Kaskazini,Hernman Batiho amesema mradi huo umechangiwa na KINAPA, wananchi, halmashauri.
Kamishna Batiho amefafanua kuwa gharama za mradi ni jumla shilingili milioni 238, 994 ,540. ambapomMchango wa TANAPA ni 214 994 540 na thamani ya mchango wa wananchi ni 24,000,000/=. Gharama hizo zinajumuisha ujenzi pamoja na ununzi wa samani na vifaa tiba.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa