Serikali mkoani Kilimanjaro imesema haitafunga wala kuzuia shughuli za dini yoyote ndani ya mkoa huo.
Msimamo huo umetangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira alipotoa salamu za serikali wakati wa kuaga miili 19 ya watu waliopoteza maisha baada ya kukanyagana katika mkutano wa kidini katika uwanja wa majengo Manispaa ya Moshi.
Mhe. Dkt. Mghwira amesema kauli hiyo ya serikali inatoka kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. " Asubuhi ya leo nilpozungumza na Mhe. Rais alisema shughulikieni mapungufu yaliyojitokeza, msifunge shughuliza dini" Alifafanua Mhe. Dkt. Mghwira.
Kufuatia maelekezo hayo, Mhe. Dkt. Mghira amesisistiza kuwa lazima watu wote waendelee kumtafuta Mungu lakini mapungufu ya kibinadamu yashughulikiwe
Aidha Mhe. Dkt. Mghwira ameagiza kuwa mikusanyiko yote itakayofanywa ndani ya mkoa wa Kilimanjaro iwe ya kidini au mikusanyiko mingine, lazima izingatie kanuni na sheria ikiwemo kuheshimu muda wa kuanza na kumaliza.
Kwa upande wao viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali waliofika katika viwanja hivyo wamesisitiza waumini wa dini zote kumtafuta Mungu bila kusahau kutumia maarifa yao ili imani zao ziswaletee madhara.
Watu ishirini waliopoteza maisha baada ya kukanyagana katika mkutano wa kidini siku ya jumamosi ya tarehe 1 mwezi wa pili 2020 katika uwanja wa majengo Manispaa ya Moshi.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa