Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira amewataka wanawake wote nchini kuwa majasiri na kujiamini wanapokuwa kwnye shughuli za maendeleo ili kuahakikisha kuwa maendeleo yanapatikana katika taifa.
Akiongea na wanawake wanaunda jumuiya ya wanawake wanaondesha shughuli za utalii nchini (AWOTTA) Mhe Dkt. Mghwira amewaambia wanawake hao kuwa huu si wakati wa kutafuta nafasi ya mwananmke katika uongozi bali ni kusimama imara katika nafasi waliyonayo ili kuhakikisha malengo yao na malengo ya taifa yanafikiwa.
Aidha mwenyekiti wa AWOTTA Bibi Marry Kalikawe amemjulisha Mhe. Mkuu wa Mkoa kuwa tayari wameanza kuona mafanikio hususan katika kubadilisha fikra za jamii na kuaminisha watu kuwa wanawake wana uwezo wa kufanya shughuli yoyote ambayo italeta tija kwa jamii kama wanavyoweza wanaume.
Amemueleza Mhe.Mkuu wa Mkoa kuwa walipowasilisha taarifa za uwepo wa AWOTTA kwenye kundi la "whatapp" la wafanyabiashara ya utalii walipata pongezi nyingi kutoka kwa wafanyabiashara wenzao ambao ni wa jinsia ya kiume na kupewa ujumbe wa heshima kutoka kwa wafanya bishara hao.
Ameongeza kuwa wanawake wameshatoka kuwa mfano wa watu wenye tabia mbaya katika jamii ikiwemo kupoteza muda katika kuendekeza tabia za umbea na ugombanishi, badala yake wameonekana ni kundi linalojikita zaidi katika kufanya shughuli za maendeleo kwa ajili ya familia zao na taifa kwa ujumla.
Wanachama wa AWOTTA walimtembelea Mhe. Dkt. Anna Mghwira ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha na kuweka mikakati ya ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro na taifa kwa ujumla.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa