Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za mkoa wa Kilimanjaro wamesisitizwa kuhakikisha kuwa wanatenga na kutekeleza bajeti za utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wananawake, vijana na watu wenye ulemavu katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021.
Akiongoza mjadala wa makadirio ya bajeti ya mkoa wa kilimanjaro kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 kwenye kiao cha arobaini na moja cha kamati ya ushauri ya mkooa RCC, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mghwira amezitaka halmashauri kuhakikisha kuwa kila halmashauri itenge kwenye bajeti na kuhakikisha fedha hizo zinafika kwaye makundi.
Aidha amewaelekeza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanavisaidia vikundi vyote vyenye utayari wa kupatiwa mikopo ikiwa ni pamoja na kuwa tayari kuwasikiliza na kuwapa miongozo ya kuifikia huduma hiyo.
Naye Mkuu wa wiyala ya Mwanga Mhe. Thomas Apson amiekieleza kikao hicho kuwa miongoni mwa changamoto wa nazokutana nazo ni pamoja na kuaminiana miongoni mwa wanavikundi vya watu wenye ulemavu hususan katika usimamizi wa fedha.
Naye katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Khatib Kazungu amewataka wakurugenzi watendaji wa halmashauri kupitia kwa umakini yaliyomo kwenye viamabatanisho vya bajeti zao ili kuhakikisha zinakuwa sahihi na zenyeauhalisia ili kuepuka kuwa na bajeti zinazotekelezeka.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa