Halmashauri za wilaya na manispaa katikia mkoa wa Kilimanjaro zimetakiwa kufanya kazi kwa umakini na weledi ili kuepukana na tatizo la hati chafu.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Khatib Kazungu wakati wa kufungua mafuzo ya maandalizi ya mipango na bajeti za halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/21 pamoja na matumizi ya mifumo kwa maafisa wa halmashauri.
Dkt. Kazungu amesema endaapo washiriki wote wa mafunzo watashiriki kikamilifu katika mafunzo hayo maboresho yataonekana kwenye kuingiza takwimu sahihi za mapato kwa mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki yaani LGRCIS pamoja na kuandaa taarifa za robo mwaka.
Aidha Dkt. Kazungu amefafanua kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo maafisa manunuzi katika kusimamamia mfumo wa kusimamia manunuzi kwa njia ya kielektroniki wa TANePs pamoja na maafisa mipango kuongezewa uwezo wa kuandaa bajeti za halmashari kwa ufanisi.
Sekretarieti ya mkoa wa kilimanjaro kupitia seksheni ya usimamizi wa serikali za mitaa imeandaa mafunzo ya siku mbili ya maandalizi ya mipango na bajeti za halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/21 pamoja na matumizi ya mifumo kwa maafisa wa halmashauri.
Akitoa shukrani kw Katibu Tawala wa Mkoa Kilimanjaro Dkt. Khatib Kazungu mwenyekiti wa washiriki wa mafunzo hayo Bw. David Rubibira amemuahidi Dkt. Kazungu kuwa washiriki wote watashiriki kikamilifu kama alivyoelekeza.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa