Halmashauri ya wilaya ya Siha imeagizwa kutumia msimu ujao wa mvua za masika kupanda miti pembezoni mwa barabara ya Sanya juu Elerai ili kutunza mazingira ya barabara hiyo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Dkt. Anna Mghwira alipokagua barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 32.
Mhe. Dkt. Mghwira amesema kazi ya Wakala wa Barabara Tanzania ,TANROADS ni kujenga na kuzitunza barabara na wameshatimiza wajibu wao, lakini kwa upande wa mazingira ni jukumu la halmashauri kuotesha miti na kuitunza ili iweze kupendezesha muonekano wa barabara na kuwawezesha wananchi kupata hewa safi kutoka kwenye miti hiyo.
"Miti itakapooteshwa pamoja na faida zingine itatunza mazingira na kupunguza vumbi pamoja na mmomonyoko wa udongo unaosababishwa na upopo." Amesema Dkt. Mghwira.
Kwa upande waake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasghauri ya wilaya ya Siha Bw.Ndaki Mhuli amesema amepokea maelekezo hayo kutoka kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa na kuahidi kuyatekeleza kwa juhudi na maarifa yote.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa