Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro amesema ameridhika na kasi na viwango vya ukarabati kituo cha afya cha karume kilichopo Useri wilayani pamoja ujenzi wa hospali ya wilaya ya Rombo.
Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya haospitali ya wilaya ya Rombo, Mhe. Dkt. Mghwira amewapongeza watumishi wa umma na mafundi wanaoshiriki katika miradi hiyo ambayo ni muhimu kwa kuhudumia afya za watu wa Rombo
Awali Mganga Mkuu wa wilaya ya Rombo Dkt. Boaz Mwakungile amemueleza Dkt. Mghwira kuwa halmashauri ya wilwya ya Rombo imepokea kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Rombo.
Dkt. Mwakungile amemueleza Mhe. Mkuu wa Mkoa kuwa fedha zilizotumika hadi sasa ni shilingi bilioni 1.33 ambazo zimetumika kukamilisha majengo ya Utawala, mionzi, jeongo la wagonjwa wa nje (OPD), kufulia, stoo ya dawa, maabara na wodi ya wazazi ambayo yapo kwenye hatua za umaliziaji.
Ameongeza kuwa mwezi Juni 2020 Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi mililioni 3000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo yaliyo kwenye umaliziaji pamoja na kuanza kwa jengo la huduma za mama na mtoto.
Aidha Dkt. Mwakungile amebainisha kuwa halmashauri iliunga mkono juhudi za serikali kuu kwa kuchangia kiasi cha milioni 10 katika ujenzi wa majengo 6 ambayo yapo kwenye hatua za ukamilishaji ambapo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 halmashauri imetenga kiasi cha milioni 48.9 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo.
Hospitali ya wilaya ya Rombo inarajiwa kuwa na majengo yasiyopungua 22 ambayo yatatumika kuhudumia wananchi zaidi laki mbili katika wilaya ya Rombo.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa