Tarehe 26 Aprili mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuwa Taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho haya yamefanyika Kimkoa kwa kuandaa Kongamano la Mafanikio ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa na watoa mada mbalimbali.
Hata hivyo, Muungano huu umejengeka kutokana na historia ya uhusiano wa undugu wa damu ya wananchi wa Tanganyika na Zanzibar, harakati za pamoja za kupigania haki na ustawi wa wananchi wa nchi zote mbili kupitia ushirikiano wa vyama vya ukombozi vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shirazi Party (ASP) katika kupigania uhuru. Mahusiano hayo yaliyowezeshwa na kudumishwa na waasisi wa Taifa letu, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ndiyo yaliyorasimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Kiliamnjrao Mhe. Nurdin Babu amesema muungano huo umesadia kujenga na kuturithisha misingi ya undugu, uzalendo, amani, upendo, mshikamano na utulivu ambavyo vimekuwa nguzo kuu ya Muungano wetu.
Mhe. Babu amesema Muungano huu umedumu kutokana na mizizi yake kujikita kwa wadau wakuu wa Muungano ambao ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia umakini mkubwa na usikivu wa hali ya juu wa viongozi wetu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza sera endelevu za Muungano na kufuatilia kwa karibu changamoto zinazojitokeza na kuzipatia ufumbuzi umekuwa chachu katika kudumu kwa Muungano wetu.
Aidha,Mhe. Babu amesema kutokana na kuimarika kwa amani, utulivu na usalama katika nchi yetu mambo muhimu yameimarika kama uchumi na ustawi wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta za elimu, afya, siasa, utamaduni na kijamii. Kuimarika huko kunatokana na uwepo wa mazingira wezeshi na mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
Aidha, Kuongezeka kwa miundombinu ya kutolea huduma ya Afya kwa kuongeza vituo vya kutolea huduma za afya ndani ya Mkoa ambavyo kwa sasa Mkoa una vituo vya kutolea huduma za afya 427 ambapo kati ya hivyo Hospitali 21, vituo vya afya 51 na Zahanati 344.
Kusambaza na kukarabati miundombinu ya umeme na kufanya vijiji na Mitaa 569 kati ya vijiji na Mitaa 579 iliyopo katika Mkoa kufikiwa na huduma ya umemepia Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu imejenga jumla ya Shule za awali na Msingi 1978, Sekondari 352, Vyuo vikuu na kati 75 ambayo imerahisisha upatikanaji wa huduma ya elimu karibu na wananchi.
Kwa upande Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Tixon Nzunda katika maadhimisho hayo amesema Tanzania ni Nchi imara isiyoweza kuyumbishwa na mtu yoyote kutokana na misingi imara iliyojengwa na Viogozi wetu.
Aidha, Nzunda amesema kuongamano hilo linawaleta pamoja wadau wa Mkoa wa Kilimanjaro lengo hasa ni kuendeleza taaluma, utafiti na ushauri katika kudumisha na kuendeleza Muungano wa Taifa letu na kujenga maarifa kwa watu nchini na Duniani kote.
Vile vile linalenga kuafakari kwa pamoja na kwa kina juu na namna bora zaidi ya kuimarisha utu, umoja,mshikamano,udugu kama Msingi imara wa Muungano wetu kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania, Africa na Dunia kwa ujumla.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa