Serikali na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjarowamepongezwa kwa kushika nafasi ya pili kitaifa katika utoaji wa huduma chakula kwa wanafunzi shuleni.
Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Bw. Charles Kabeho baada ya kuweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari ya wasichana Machame iliypo wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Kabeho amengeza kuwa utoaji wa chakula kwa wanafunzi una faida kubwa hususani kupunguza utoro na kuongeza ufaulu.
Aidha kabeho amewakumbusha wazazi kuwa sera ya utoaji wa elimu bila malipo unaotekelezwa na serikali haiondoi wajibu wa mzazi na mlezi katika kumgharamia mtoto mahitaji yake mengine ya elimu kama vile sare, madaftari, viatu pamoja na chakula.
Kabeho amewaasa wazazi na walezi kuheshimu makubalino wayoweka hususan kweny taratibu wanazojiwekea katika kuchangia chakula cha watoto.
Amefafanua kuwa suala la kuchangia chakula kwa ajili ya watoto ni hiari lakini mara makubaliano yanapofikiwa na wazazi na walezi kwa umoja wao kila mmoja anawajibika kutekeleza makubaliano hayo.
Mkoa wa njombe umeshika nafasi ya kwanza katika utoaji wa huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa