Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2025, Ndg. Ismail Ussi ametoa wito kwa mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa daraja la Mandaka Uzungo lililopo wilayani Mwanga kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa ili kurejesha mawasiliano muhimu katika eneo hilo.
Ametoa wito huo leo Julai 1,2025 wakati wa kukagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi huo, Ndg. Ussi ameendelea kusema serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa madaraja, barabara na miundombinu mingine.
Ameeleza kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa Mwanga kwa kuboresha usafiri na kuongeza fursa za kiuchumi kwa jamii inayozunguka eneo hilo.
Aidha, Ndg. Ussi amewasihi wananchi wa eneo hilo kutunza miundombinu hiyo kwa kuzuia vitendo vya uharibifu, akisisitiza kuwa serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuilinda kwa maslahi ya wote.
Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mhandisi anayesimamia ujenzi M/S EIMA GENERAL CAMPANY Ltd na kusimamiwa na TARURA wilaya ya Mwanga alieleza kuwa gharama za ujenzi wa daraja hilo ni zaidi ya shilingi milioni 319, huku pia kukijengwa barabara ya kuingia katika eneo hilo yenye urefu wa kilomita 1.2.
Mradi huo unatajwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Mwanga, kwani mbali na kurahisisha mawasiliano, pia utafungua fursa mpya za biashara na kuinua uchumi wa eneo hilo.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa