Makatibu Tawala wa Wilaya katika mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kuwapa ushirikiano maafisa tarafa ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Akizungumza baada ya kugawa pikipiki 12 zilizoletwa na serikali kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa Taraf ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira amesema pikipiki hizo zimeletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kama utekelezaji wa ahadi yake kwa maafisa tarafa ilipokutana nao Ikulu jijini dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Anna Mghwira amefafanua kuwa lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi ya kuwapa pikipiki maafisa tarafa hao ni kuwarahisishia watumishi hao wa umma utendaji wao kila siku.
Mhe.Dkt. Mghwira amesisistiza kuwa ni lazima kila Katibu Tawala wa Wilaya ahakikishe pikipiki hizo zinakuwa na mafuta ya kuwatosheleza kwenda vijini kuwatumikia wananchi kwani miongoni mwa njia za kumpima mtumishi kiutendaji ni pamoja na kuzingatia uwezeshwaji anaopatiwa na msimamizi wake wa kazi.
Aidha Mhe. Dkt. mghwira amesema ni mategemeo yake kuwa atakapofanya ziara katika wilaya zote Maafisa Tarafa watashiriki ipasavyo na ni mategeeo yake ni kuwa na maafisa tarafa wenye ufahamu na uelewa wa kutosha juu ya kero,changamoto na fursa za wananchi wanaowahudumia kwani kwa sasa kila Afisa Tarafa ameshawezeshwa kuwafikia wananchi.
Kuhusu matumizi sahihi ya pikipiki hizo Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema si ruhusa kwa Maafisa Tarafa kuzitumia pikipiki hizo kwa shughuli ambazo si za umma ikiwa ni pamoja na kubebea abiria kama bodaboda.
Mkoa wa Kilimajnaro wenye tarafa 30 ulikuwa na upungufu wa pikipiki 10 na kubahatika kupata nyongeza pikipiki 12 na kufanya kuwa na ziada ya pikipiki 2 ambazo zitapangiwa majukumu mengine.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa