Taharuki ilitanda katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimajnaro na maeneo ya jirani asubuhi ya leo wakati Kikosi cha zimamoto na uokoaji kilpofanya majaribio ya uelewa wa watu katika kujinusuru na majanga kama ya moto pindi yanapotokea katika majengo yao au mahala pa kazi.
Watumishi wa serikali pamoja na wateja mbalimbali walikuwa ndani na ofisi ya mkuu wa Mkoa na maeneo jirani walionekana kutawanyika huku na kule ili kujinusuru na hatari ambayo ingeweza kuwapata baada ya kusikia king'ora cha kuashiria majanga kiliposikaka katika jengo hilo.
Akiongea na waandishi wa habari katika eneo hilo Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba amesema zoezi hilo lilikuwa ni kupima utayari wa watumishi katika kukabiliana na majanga hususan moto.
Mhe. Warioba amesema pamoja na mambo mengine wananchi wamepimwa uelewa wao juu ya kufuata maelekezo ya wataalam wa ukoaji ikiwemo kuelekea maeneo salama yaani assemby points.
Naye Muwakilishi ya Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro Mkaguzi Msaidizi Abdulwahab Mtazigwa amesema zoezi hilo ni la kawaida la kupima utayari wa wananchi katika kuitikia miito ya moto.
Aidha ameongeza kuwa wametekeleza zoezi hilo kwa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba ili kupima matokeo ya elimu ya kujiokoa na majanga ya moto ambayo ilishatolewa kwa watumishi wa ofisi hiyo kwa njia ya nadharia hapo awali.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa