Serikali mkoani Kilimanjaro imethibitisha kuwa mahindi yanayozalishwa nchini yana ubora na salama kwa watumiaji.
Akiongea na waandishi wa habari alipotembelea mpaka wa Holili unaunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya Mkuu wa Mko wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira amesema bidhaa hiyo imekaguliwa na kupimwa na watalaam wanahusika na masuala ya usalama wa chakula likiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), hivyo mahindi hayo ni bora na salama kwa watumiaji.
Mhe. Dkt. Mghwira ametoa wito kwa wafanyabiashara na wachuuzi wa mahindi kufika ofisi ya mkuu wa mkoa au ofisi ya mkuu wa wilaya ya Rombo kwa ajili ya kupata taratibu za kununua bidhaa hiyo kwani tayari serikali imeshaandaa maeneo mawili ya kukusanya na kuuza bidhaa hiyo.
Aidha Mhe. Dkt. Mghwira amewataka watumishi wa taasisi za umma zinazosimamia biashara katika mpaka pamoja na wafanyabiashara wote kujiepusha na biashara ya magendo ikiwemo utoroshaji wa mahindi na nafaka nyingine kupia njia zisizo rasmi (njia za panya) kwani kufanya hivyo kunasabisha serikali kukosa takwimu za nafaka zinazozalishwa nchini, uuzwaji wake nje ya nchi pamoja na kiasi kinachotumika nchini.
Amesissitiza kuwa yeyote atayekamatwa kwa kuhusika na usafirishaji wa chakula na bidhaa zingine kwa njia ya magendo atakapokamatwa asilamike kama anaonewa kwani hatua kali za kisheria zitachuliwa dhidi yake .
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa