Mwenge wa Uhuru umepokelewa Mkoani Kilimanjaro Juni 20, 2023 kutoka Mkoani Tanga na
Jumla ya miradi 45 kutoka halmashauri zote za Mkoa wa Kilimanjaro itapitiwa na Mwenge wa Uhuru.
Akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema, Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Kilimanjaro utapata fursa ya kupitia jumla ya miradi 45 ambayo inapatikana katika Halmashauri zote saba za Mkoa wetu. Katika miradi hiyo 13 ni ya kufunguliwa/kuzinduliwa, 15 kuwekewa mawe ya msingi, 17 ni ya kukaguliwa, Fedha zilizotumika na zinazoendelea kutumika kukamilisha miradi hiyo yote ni Shilingi Bilioni thelathini, milioni mia tatu na hamsini na mbili, mia nane na ishirini na sita elfu, mia saba na themanini na sita na senti thelathini na tano (30,352,826,786.35).
Amesema Mwenge wa uhuru, utapata fursa ya kuona na kutembelea juhudi mbalimbali zinazofanywa na vikundi vya vijana, walemavu na wanawake katika kuzalisha mali ili waweze kujiendeleza kiuchumi, pia utazindua klabu za kupambana na Rushwa na kutembelea maonesho mbalimbali ya shughuli za elimu.
Aidha, Mhe. Babau amesema katika kutekeleza miradi hiyo iliweza kuchangiwa na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka Serikali Kuu ambapo ilichangia shilingi 24,402,037,912.30 (shilingi bilioni ishirini na nne, milioni mia nne na mbili, thelathini na saba elfu, mia tisa na kumi na mbili na senti thalathini) na Michango ya fedha na nguvu za wananchi ni shilingi 333,182,572.00 (Shilingi Milioni mia tatu na thelathini na tatu, mia moja themanini na mbili, na mia tano na sabini na mbili); kwa uapnde wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa zimechangia shilingi 4,091,143,386.05 (Shilingi bilioni nne, milioni tisini na moja, mia moja arobaini na tatu elfu, mia tatu na themanini na sita na senti tano); bila kuwasahau Wawekezaji (Wafadhili mbalimbali) ni shilingi 1,526,462,916.00 Shilingi bilioni moja, milioni mia tano na ishirini na sita, mia nne na sitini na mbili elfu, na mia tisa na kumi na sita).
Hata hivyo Miradi yote hii ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 imegusa sekta zote ambazo ni elimu miradi 9, Afya miradi 9, maji miradi 7, Utunzaji wa mazingira miradi 7, barabara na madaraja miradi 6, Vijana Miradi 5, na miradi mengineyo 2. Miradi hii iliyotekelezwa imesaidia kuzalisha ajira za muda kwa wananchi 12,366. Hapana shaka kuwa, Mwenge wa Uhuru utakapokuwa unakimbizwa hapa Mkoani utaendelea kuimarisha umoja na mshikamano tulionao.
Babu amesema Mkoa wa Kilimanjaro unatambua na kuthamini umuhimu wa hifadhi ya mazingira pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kuendelea kutekeleza maagizo mbalimbali ya Serikali kuhusu Usimamizi wa Maliasili na Mazingira kulingana na Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo na maelekezo yanayotolewa na Serikali ambapo Mkoa kwa kushrikiana na Wadau mbalimbali wa Uhifadhi ndani ya Mkoa (KINAPA, TFS, Bonde la Pangani, RUWASA, MUWSA n.k), pia kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Sera ya Mazingira ya Mwaka 2021 sambamba na utekelezaji wa Agizo la serikali katika upandaji wa miti 1,500,000 kwa kila halmashauri kwa mwaka kupitia zoezi la Upandaji Miti na utunzaji wa vitalu vya Miche. Jumla ya miti 6,765,328 imepandwa kwenye maeneo ya taasisi mbalimbali, vyanzo vya maji na maeneo ya wazi kwa mwaka 2022/23.
Vile vile Mhe. Babu amesema, Mkoa una jumla ya vyanzo vya maji 579. Kati ya hivyo, vyanzo 125 vinatumika kuhudumia skimu za maji 192. Vyanzo 51 vina hali nzuri vikiwa na uzio na haviko katika athari ya kuvamiwa na shughuli za kibinadamu. Vyanzo 74 vinatoa huduma lakini vimevamiwa na binadamau katika shughuli za kilimo ambapo tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa kwa kutumia sheria ndogondogo za Halmashauri pamoja na sheria ya Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004.
Kwa upande wa Lishe bora na athari zitokanazo na lishe duni Mkoa kupitia Halimashauri umeendelea kupanga fedha kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani ili kutekeleza afua za lishe zinazolenga kuboresha hali ya lishe katika jamii. Mkoa kupitia Halmashauri zake umetumia Tshs. 229,943,024.00 kwa kipindi cha Julai 2022 - Machi, 2023 sawa na asilimia 69 ya Tshs. 331,909,280.00 zilizopangwa kutekeleza afua za lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa mwaka wa fedha 2022-23.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa