MATUKIO 13 YATAKAYO FANYIKA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA FIMBO NYEUPE DUNIANI MKOANI KILIMANJARO
Maandalizi ya maadhimisho ya yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro tarehe 21-25 Octoba,yameanza rasmi Agosti 13,2024 katika kikao cha kwanza cha maandalizi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amewataka wajumbe wote wa kikao pamoja na wadau waliyopo Mkoani Kilimanjaro kushiriki vema katika maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Fimbo Nyeupe Dunia lengo ni kufanikisha tukio hilo kikamilifu linaloratibiwa na chama cha watu wasioona Tanzania (TLB).
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Kiseo Yusuph Nzowa amebainisha matukio muhimu 13 yatakayofanyika katika maadhimisho hayo ni pamoja na kupandisha fimbo nyeupe kwenye Mlima wa Kilimanjaro, kutembelea kaburi la Hayati Reginald Mengi,maonyesho mbalimbali kwa watu wasioona ,upimaji wa macho na magojwa sugu pia uchangiaji damu, maonyesho ya teknolojia kwa wasioona, maonyesho ya matumizi ya komputa ,maandamano kwa wasioona, matumizi ya simu janja kwa wasioona,ugawaji wa miti kwa wanachama wasioona,usajili wa wanachama wapya kwa wasioona,ugawaji wa Fimbo Nyeupe kwa wasioona na kuendesha midahalo.
Naye, Kaimu Katibu wa Chama Cha Wasioona Bw. Loata Mollel amesema Chama Cha watu wasioona ni Chama cha kiraia ambacho kimeanzishwa mwaka1964 kikasajiliwa na Wizara ya mambo ya ndani mwaka1972 ambacho kimefikisha miaka 60 huku jukumu kubwa ya chama hiki ni kutetea Watu wasioona pia kuchochea upatikanaji wa huduma muhimu Kwa watu watu hao.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa