Wananchi wilayani Moshi wametakiwa kutumia vema haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi watakaoshirikiana vema na serikali katika kuwaletea maendeleo.
Akihutubia katika mikutano ya kampeni katika viwanja vya Kibosho kirima wilayani Moshi na Majengo katika manispaa ya Moshi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wananchi wilayani Moshi kuhakikisha wanachagua viongozi watakaoshiriki kwa ukamilifu vikao vyote vya kufanya maamuzi ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Mhe. Majaliwa amewaambia wananchi hao kuwa hawatajuta endapo watachagua viongozi ambao hawatatoka kwenye mikutano ya bunge na halmashauri hususan katika vipindi vya kujadili na kupitisha bajeti za maendeleo yao.
Mhe. Majaliwa ameeleza kuwa matatizo na kero za wananchi wa wilaya ya Moshi amezijua kupitia taarifa anazozipata kupita wakurugenzi wa halmashauri lakini wabunge wa majimbo hayo wamekuwa hawafikishi kero na mahitaji yao kwa viongozi wakubwa wa serikali na wanapotakiwa kufikisha matatizo hayo kupitia vikao vya bunge wamekuwa wakisusia na kutoka kwenye kumbi za mikutano.
Aihha Mhe Majaliwa ameataka wananchi kuhakikisha wanapigia kura wagombea wote wa Chama cha mapinduzi ili iwe rahisi kuwatumikia ."Wapigieni kura wagombea wa ubunge wa CCM, wapigieni kura wagombea wa udiwani wa CCM na mumpigie kura Mhe. John Magufuli ili mpate viongozi watakaoshirikiana kikamilifu ili kwaletea maendeleo".
Waziri Mkuu Majaliwa amefanya mikutano ya Kampeni katika kata ya Kirima wilayani Moshi na kumuombea kura ProfesaPatrick Ndakidemi wa Jimbo la Moshi vijijini kupitia CCM na Priscuss Tarimo mgombea ubunge wa jimbo la Moshi mjini kupitia CCM.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa