Katibu Tawala Msaidizi wa Uchumi na Uzalishaji, Dkt. Emmanuel Lema, akiambatana na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko, Ndg. Stephen Michael, wameendesha mafunzo ya vitendo kwa wadau wa tasnia ya ngozi katika Kiwanda cha Kilimanjaro International Leather Industries.
Mafunzo hayo yalihusisha wadau mbalimbali wakiwemo wachunaji, wasindikaji, wasimamizi wa machinjio, na wafanyabiashara wa ngozi. Kupitia mafunzo hayo, washiriki walipata nafasi ya kuona kwa karibu hatua mbalimbali za uchakataji wa ngozi hadi kuwa bidhaa inayoweza kuuzwa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Ndg. Stephen Michael aliwataka wadau kuhakikisha mnyororo mzima wa thamani ya zao la ngozi unaboresha kwa pamoja ili kuhakikisha viwanda havikosi malighafi za kutosha.
Kwa upande wake, Dkt. Lema aliishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuendelea kutekeleza mkakati wa kuboresha zao la ngozi mkoani Kilimanjaro. Pia aliahidi kusimamia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa ili kuongeza tija na ushindani wa zao hilo katika soko la ndani na la kimataifa.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa