Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kupitia Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, imefanya ufuatiliaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Mashirika yaliyotembelewa ni pamoja na TAWREF na KIVUCE yanayotekeleza shughuli zake katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, YEPAO na Courage World Wide yanayotekeleza miradi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, huku wilayani Hai ni VOEWOFO na Kilimanjaro New Vission Sober House pamoja na DSW & HRNS inayopatikana wilayani Siha.
Akizungumza kuhusu lengo la ufuatiliaji huo, Wakili kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Tatu Ally, alisema kuwa hatua hiyo inalenga,
Kusaidia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayotekeleza afua kwa makundi yaliyo hatarini, hususan wasichana balehe na wanawake vijana, kuhakikisha yanazingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya uratibu wa NGOs nchini.
Pamoja na Kubaini changamoto na mapungufu katika utekelezaji wa miradi ili kutoa ushauri na kutafuta suluhisho sahihi na Kufuatilia matokeo ya miradi ili kuhakikisha afua zinazotekelezwa zina manufaa kwa jamii na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho.
Vile vile Kuyajengea uwezo mashirika hayo kupitia mafunzo ya Mfumo wa Uratibu wa NGOs (NIS), Mwongozo wa Uratibu pamoja na Mkakati wa Taifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NSNS) 2022/2023 – 2026/2027.
Aidha,Ufuatiliaji huu ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha mashirika yasiyo ya kiserikali yanaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, uwazi na kwa manufaa ya jamii hususan makundi yaliyo katika mazingira hatarishi.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa