Mkoa wa Kilimanjaro umetajwa kama mkoa unaouhitaji zaidi mpango wa kunusuru kaya masikini unaosimamiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf ukilinganishwa na mikoa mingine.
Hayo yamesemwa na waziri wa nchi ofisi ya rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Kapt.(Mst.) George Mkuchika baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika mkoa wa Kilimanjaro.
Mhe. Mkuchika amesema ufinyu wa ardhi katika mkoa wa Kilimanjaro unapelekea mwananchi masikini mwenye nguvu na aliyetayari kujishughulisha hata kwa kilimo cha kujikimu hushindwa kufanya hivyo kwani kila kipande cha ardhi katika mkoa wa Kilimanjaro kinamilikiwa na mtu.
Kufuatia hali hiyo Waziri mkuchika amesema serikali inawaangalia kwa jicho la pekee watu wenye hali duni za kimaisha katika mkoa wa kilimanjaro kwani hawana fursa ya ardhi kama ilivyo katika mikoa mingine.
Mhe mkuchika amewataka waratibu wote wa Tassaf mkoani Kilimanjaro kuhakikisha kuwa kila mwananchi mwenye sifa ya kunufaika na mpango huo anafikiwa na kunufaika kwa mujibu wa taratibu za Tassaf na uwezo wa mfuko.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo mratibu wa Tasaf mkoa wa Kilimanjro Bw. Apolinary Seiya amesema Katika awamu zote kumi na tisa (19) za malipo kiasi cha Shilingi Bilioni 21 zililipwa kwa walengwa.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa