Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira amelipongeza Shirika la Hifadhi za Taifa, TANAPA kwa kuwa wepesi wa kupokea maombi ya watu na mamlaka mbalimbali na kuyafanyia kazi na hatimaye kufanya utekelezaji unaotoa matokeo chanya.
Akiongea wakati wa kupokea mradi wa nyumba ya walimu wa shule ya msingi Malimeni kata ya Vunjo Magharibi wilayani Moshi, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Dkt. Anna Mghwira amesema TANAPA kupitia hifadhi ya taifa ya mli ma Kilimanjaro, KINAPA imepokea na kufanyia kazi changamoto ya nyumba za walimu katika mkoa wa Kilimanjaro na kufanya maamuzi yatakayopelekea kusukuma mbele maendeleo ya elimu katika mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa mujubu wa Kamishna Mwanadamizi wa TANAPA Kanda ya Kaskazini, Herrman Batiho mradi wa nyumba ya walimu wa shule ya msingi Malimeni umegharimu jumla shilingi za kitanzania milioni 120.6 na kuwataka wananchi kufuata sheria zinazolinda hifadhi ili vitendo vya uchonaji koto, ujangili, uchungaji wa mifugo visifanyike ndani ya hifadhi ili hifadhi iwe endelevu kwa maslahi ya umma.
Kuhusu utunzji wa Mazingira Mhe. Dkt. Anna Mhgwira amesema KINAPA ni mfano wa kuigwa kwani sanamu ya mlima waliyoijenga katika makutano ya barabara kuu inayoelekeaa mkoani Arusha na Mtaa wa Florida haitawavutia watalii tu kupanda mlima Kilimanjaro bali itaongeza ubora wa mandhali ya Manispaa ya Moshi.
TANAPA kupitia hiafadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro KINAPA imejenga sanamu ya mlima Kilimanjaro katika manispa ya moshi yenye maelezo muhimu kuhusiana na historia, njia za kupandia mlima na taarifa muhimu kuhusiana na hifadhi hiyo.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa