Wananchi wa Mkoa wa Kiilimanjaro hasa wanaoishi kwenye vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro KINAPA wametakiwa kuthamini mchango wahifadhi hiyo katika kujitoa kwenye kuchangia maendeleo ya elimu ndani ya mkoa wa Kilimanjaro.
Akiongea baada ya kupokea mradi wa madarasa mawili, ofisi ya mwalimu,madawati pamoja na samani za ofisi zilizotolewa na KINAPA kwa shule ya msingi Mweka wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira, amesema kuchangia miradi ya maendeleo ikiwemo elimu ni jukumu la jamii nzima hivyo KINAPA wanaonesha mfano wa kuigwa katika kuchangia maendeleo.
Kuhusu ubora wa vyumba vya madara pamoja na ofisi ya mwalimu Mhe. Dkt. Mghwira amesma ameridhishwa na ubora wa majengo hayo kwani ubora wa mradi unaendana na thamani."Haya ndiyo madarasa yanayotakiwa katika kutoa elimu, hata ofisi ya mwalimu ndivyo inavyotakiwa iwe pamoja na samani za ndani ya ofisi".Alisema Mhe.Dkt. Mghwira.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Ujirani Mwema Kamishna Mwanadamizi wa TANAPA Kanda ya Kaskazini, Herrman Batiho amesma mradi wa vyumba vitatu vya madarasa, ofisi ya mwalimu, madawati 72 pamoja na samani za ofisi ambazo ni meza saba, viti vinane na makabati matano, katika shule ya msingi Mweka umetekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la hifadhi za taifa TanzaniaTANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro KINAPA,wananchi na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.
Aidha Kamishna Batiho amefafanua kuwa mradi huo wenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 123,370,760 umetekelezwa kwa TANAPA kuchangia asilimia 70 ambayo ni shilingi za kitanzania milioni 120,490,760 na mchango wa jamii ni shilingi za kitanzania 2,880,000 sawa na aslimia 30.
Kamishna Batiho ameongeza kuwa wananchi wamechangiakwa kutoa nguvu kazi, malighafi pamoja na ufundi huku Halmashauri ya wilaya Moshi ikichangia ramani ya mradi, maandalizi ya gharama halisi za mradi yaani BOQ na kutoa ushauri wa kitaalam.
Akisoma risala ya shukrani kwa serikali na Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA, mtendaji wa kijiji cha Mweka, Sophia Sanga amesema wanakijiji wanatambua na kuthamini uwepo wa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kama jirani yao mwema anayewajili.
Katika wilaya ya Moshi KINAPA inatekeleza miradi ya mbalimbali ya maendeleo kwenye vijiji kumi kwa lengo la kutekeleza nia ya hifadhi ya kutoa sehemu ya mapato yake kwa jamii ili jamii inufaike na mapato yanayotokana na shughuli za uhifadhi ili na wao washiriki kuunga mkono juhudi za serikali katika kushriki kikamilifu katik ashughuli za uhidafadhi.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa