Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2025 Ndg. Ismail Ali Ussi ameweka jiwe la msingi kwenye mradi mpya wa Maji wa Mroyo - Kizangaze uliopo katika kata ya Maole wilayani Same ambao utahudumia wananchi zaidi ya elfu tatu katika kata hiyo pamoja na vijiji jirani.
Akizungumza na Wananchi wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika mradi huo Ndg.Ussi amesema Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan itaendelea kujali wananchi katika kuboresha miundombinu ya maji kupitia kampeni ya kumtua mama Ndoo kichwani ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya Mjini na Vijijini.
Pia ameipongeza mamlaka ya maji safi na salama Wilaya ya Same kwa kuendelea kutekeleza vyema miradi ya maji cha kiwango cha hali ya juu katika wilaya hiyo.
Kwa upande wake,Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Kasilda Mgeni ameeleza umuhimu wa mradi huo kwa wananchi ambapo awali walitembea umbali mrefu kufuata maji hali iliyochangia kuongezeka kwa migogoro ya Ndoa katika eneo hilo.
Aidha,Mradi wa Maji wa Mroyo - Kizangaze unagharimu shilingi zaidi ya bilioni 1 ambapo hadi kufikia sasa ujenzi umefikia asilimia 79.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa