Wananchi Wilayani Siha wametakiwa kuwekeza kwenye kilimo ambacho kitaleta tija kwa wananchi sambamba na kutunza mazingira.
Akizungumza na Wananchi baada ya kutembelea shamba la Karanga Mti (Makadamia Nuts) linalomilikiwa na Kampuni ya Namuai Farms Ltd katika Kijiji cha Namwai Wilayani Siha, Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine Mwambashi amesema amevutiwa sana na uwekezaji katika shamba hilo kwani wakulima hao mbali ya kupata faida kiuchumi jamii itaendelea kunufaika hewa nzuri itayoletwa na miti ya zao hilo.
Awali akitoa taarifa ya shamba hili Msimamizi Mkuu wa Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 2410 Bw. Abdul Sariko , amesema mimea hiyo ina uwezo wa kudumu kwa zaidi ya miaka arobaini tangu kuoteshwa endapo itatunzwa vizuri.
Bw. Sariko ameongeza kuwa uwekezaji katika shamba hilo uliogharimu shilingi bilioni 8.6 umetoa ajira za kudumu kwa wananchi 11 na ajira za muda mfupi kwa wananchi zaidi 50 ambapo wanufaika wote wa ajira ni watanzania.
Aidha amefafanua kuwa hadi sasa tayari tan 4 zimevunwa na zoezi la uvunaji bado linaendelea ambapo hadi kufikia 2022 wakulima hao wanatarajia kuvuna tani zipatazo 275.
Kuhusu soko Bw. Sariko amesema ni nzuri ambapo limekuwa likiimarika kila siku katika nchi za China, Afrika ya Kusini, Marekani na Kenya.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa