Jumla ya miradi yote 45 yenye thamani ya Tshs. Bilioni 30.35 iliyopititiwa na Mwenge wa Uhuru imefunguliwa,kuzinduliwa,kuwekewa mawe ya msingi na kukaguliwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim amepongeza Uongozi wote wa Mkoa wa Kilimanjaro na Halmashauri kwa ujumla kwa usimamizi mzuri wa miradi iliyokidhi vigezo na viwango vinavyotakiwa na kwa upangaji mzuri wa nyaraka na wataalamu kutoa ushirikiano katika ukaguzi wa miradi.
Ametoa pongezi hizo wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Kilimanjaro kwenda Mkoa wa Arusha katika viwanja vya Tingatinga Wilayani Longido.
Abdalla amesema miradi yote 45 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru hakuna uliokataliwa hii ni ishara nzuri ya ushirikiano uliopo kati ya viongozi wa ngazi tofauti tofauti katika kuleta maendeleo ya nchi.
Akiwasilisha taarifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Kutoka Mkoa wa Kilimanjaro kwenda Mkoa wa Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema mwaka huu Mkoa umezingatia vigezo vyote vilivyobainishwa kwenye muongozo hii ndio sababu ya kupata matokeo mazuri katika miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru.
Mhe. Babu amesema, Mwenge wa Uhuru ulitembelea miradi ya elimu 9, afya miradi 9, maji maji 7, utunzaji wa mazingira miradi 7, barabara miradi 6, maendeleo ya vijana miradi 5 na miradi mengineyo 2 na ulipata fursa ya kuona na kutembelea miradi mbalimbali ya makundi mbalimbali ya vijana wenye ulemavu na wanawake ambao wamedhamiria kuzalisha mali na kujiendeleza kiuchumi. Vile vile umezindua klabu za kupambana na Rushwa, Madawa ya Kulevya, Malaria,Uhifadhi na uendedlezaji wa mazingira.
Ameendelea kusema katika kipindi cha mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani hapa katika kutekeleza kauli mbiu ya Mwenge 2023 “Tunza Mazingira, okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa” Mkoa ulijiwekea lengo la kuhakikisha miradi yote itakayopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 kabla na wakati wa mbio hizo miti inapandwa na hivyo kupelekea jumla ya miti 7,857 kupandwa. Aidha, Serikali na Wananchi wamedhamiria kurudisha uoto wa asili wa Mkoa wa Kilimanjaro hivyo wamepanda jumla ya miti 6,765,328 katika maeneo ya taasisi mbalimbali, vyanzo vya maji na maeneo ya wazi kabla ya Mwenge kupita kwa kuzingatia Sera, kanuni na Taratibu za uhifadhi wa mazingira.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa