Mkoa wa Kilimanjaro umepokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Tanga Juni, 6 katika Kijiji cha Bendera, Kata ya Bendera Wilayani Same.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Kilimanjaro unatarajia kutembelea, kufungua/kuzindua na kukagua jumla ya miradi 38 ya maendeleo ikiwa na thamani ya Tshs. 13,670,634,422.60 hadi kukamilika katika halmashauri zote saba za Mkoa.
Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Tanga, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai amesema miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru imegusa katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu itakua miradi 9, Afya miradi 10, kwa upande wa Maji na Utunzaji mazingira miradi itakuwa 6, katika sekta ya Barabara na pamoja na Madaraja miradi itakuwa 6, vijana miradi 5, na miradi mengineyo itakuwa 2.
Aidha, katika operesheni ya zoezi la Anuwani za makazi kwa Mkoa wa Kilimanjaro hadi kufikia mwezi Mei, 2022 jumla ya anuwani 421,970 zimesajiliwa sawa na asilimia 100.45 ya lengo la kusajili anuwani 420,067. Jumla ya barabara 13,205 zimetambuliwa na kupewa majina ikilinganishwa na malengo ya barabara 14,896 yaliyokuwa yamewekwa hapo awali.
Kwa upande wa zoezi la Sensa Mkoa umepokea jumla ya maombi ya watu 27,446 kwa ajili ya ajira ya Sensa kwa Makarani, wasimamizi wa maudhui na wasimamizi wa TEHAMA na hii ni kutokana na tangazo lililotolewa na Serikali la kuwasilishwa kwa maomib hayo mwezi 5,2022 na kumalizika 19,mei 2022.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa