Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, umezindua ofisi ya kijiji cha Ngulu kilichopo kata ya Kwakoa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro ikiwa ni hatua za serikali za kuboresha mazingira ya watumishi katika utendaji kazi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, julai 1 kiongozi wa mbio za Mwenge, Ismail Ali Ussi amesema serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya watumishi ili wananchi waweze kupata huduma kwa haraka na kwa wakati.
Amesema Mwenge huo umepita kwa lengo kuonyesha upendo kwa wananchi, kurejesha matumaini na kuleta imani iliyokuwa imepotea.
"Tumekagua jengo hili la ofisi ya kijiji cha Ngulu, tumejiridhisha na nyaraka, ubora hakika jengo limejengwa kwa viwango vinavyostahili na thamani ya pesa imeonekana. Natoa rai kwa viongozi kuwa ofisi hizi zitumike katika kuleta mabadiliko kwa wananchi kwa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua , zitakazowashinda hakikisheni mnapeleka kwa mkuu wa wilaya au mkoa, nilazima wananchi wapate majawabu ya matatizo yao,"
Aidha aliwataka watumishi watakaofanya kazi katika eneo hilo kufanya kazi kwa uwaminifu na kwa haraka ili kuwasaidia wananchi kujikita katika shughuli za kiuchumi na kuleta maendeleo.
Akimkaribisha kiongozi huyo, mkuu wa wilaya ya Mwanga Bi. Rukia alisema wananchi hao wataweza kutatuliwa matatizo yao katika eneo hilo.
Alisema awali walikuwa na ofisi ya kijiji isiyokidhi mahitaji jambo lililokuwa likiwakosesha viongozi raha wakati wa utendaji kazi wao.
Akisoma taarifa ya mradi huo, Angela Kilawe alisema jengo hilo liligenjwa kwa gharama ya milioni 56
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa