Mwenge wa Uhuru umekabidhi hundi ya Tshs. 3 kwa kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu Mama Kevina ikiwa ni sehemu ya michango ya fedha za Mwenge katika halmshauri ya Same.
Akikabidhi hundi hiyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava wakati alipotembelea kituo hicho ametoa wito kwa wazazi wanaopelekea watoto kwenye vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji maalumu kuwatembelea kila wakati ili kujua maendeleo yao na wanapopata nafuu wanaweza kuwarudisha nyumbani kuendelea na maisha ya kawaida.
Hata hivyo, Mnzava amewataka wananchi wote nchi nzima kutowaficha watoto wenye mahitaji maalumu na kuacha tabia wa kuwanyanyapaa na kuwatenga kwani na wao ni binadamu kama watoto wengine.
Akisoma taarifa ya kituo hicho Maria Kijangwa Raymomd amesema kituo hicho kilianzishwa na shirika la kidini Jimbo Katoliki Same chini ya Dada wadogo wa Mt. Fransisko wa Assis mwaka 2008 kwa lengo la kutoa huduma mbili ikiwa ni uchunguzi ambapo hufanywa na watumishi wa kituo hicho kwa kushirikiana na watumishi wa Halmashauri kwa kutembea kwenye makazi ya wananchi ili kuwabaini watoto wenye mahitaji maalumu na kuwapa elimu wazazi na walezi ya viashiria vya ulemavu. Huduma ya pili ni matibabu ya watoto hao ambayo yanahusisha mazoezi ya viungo ambapo wazazi na walezi huelekezwa namna ya kuwasaidia watoto hao.
Vile vile Maria amesema takribani watoto walemavu 600 wameweza kufikiwa majumbani kupatiwa huduma huku 44 wakiwa kituoni kwa ajili ya kupatiwa elimu, malezi na uangalizi maaalumu.
Ameendelea kusema watoto 12 wamesaidiwa kupata elimu katika shule ya Sekondari na 33 elimua ya Msingi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni amesema kituo hicho kimekua mkombozi kwa wananchi wa halmashauri ya Same kwa kuwasaidia wazazi na walezi kujengewa uelewa wa namna ya kuwajali watoto wenye mahitaji maalumu kama vile watoto wenye ulemavu, kuongea na wenye utindio wa ubongo.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa