Maelfu ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania, wamejitokeza katika uwanja wa C.D Msuya uliopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kuaga mwili wa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri mkuu (Mstaafu) Hayati Cleopa David Msuya(94).
Pamoja na hilo, walikuwepo viongozi waandamizi wa serikali ya awamu ya sita akiwemo Waziri wa Nchi, Ofsi ya Waziri Mkuu , Sera Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi pamoja Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Sera Uratibu na baraza la wawakilishi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma.
Mwili wa Hayati Msuya, uliwasili mkoani Kilimanjaro Mei 12 majira ya saa mbili asubui kwa ndege maalumu ukitoke jijini Dar es Salaam na kulakiwa na maelefu ya watu wakiwemo viongozi wa Serikali wa ngazi mbalimbali pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.
Ulitembezwa kwa mwendo wa pole na gari maalumu liloongozwa na jeshi la wananchi wa Tanzania na kupitia barabara Kuu ya Arusha -Moshi hadi katika viwanja vya C.D MSUYA vilivyopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro na kulakiwa na maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa dini.
Akitoa mahubiri katika ibada iliyoongozwa katika viwanja vya C.D Msuya wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro Askofu mteule wa kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Mwanga, Dk. Daniel Meno aliwataka wananchi kujitambua na kuwaepuka viongozi watakaokuja kwa ajili ya kuwalaghai hasa kipindi tunapoelekea Uchaguzi mkuu 2025.
Alisema kwa sasa wapo viongozi wengi wenye tabia za kuja kununua kura ili kujipatia madaraka na kujifufaisha wenyewe kwa maslai yao na kuwataka wananchi kuona thamani ya kura yao.
"Tuwe makini, baba yetu Msuya ametufundisha uwajibikaji, uadilifu na ukweli na alikuwa kiongozi wa kweli mwenye kuleta mageuzi.Kwa sasa kuna viongozi wa aina mbili, moja ni wale wanaouliza watapata nini na wale wanaowaza wataacha nini, ni wajibu wetu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu 2025 kupima na kuchagua viongozi wenye tija.
"Wanamwanga tuendelee kushikamana, tusikubali kubaguana kwa sababu yoyote ile ikiwemo kabila zetu na dini zetu,vyeo, elimu zao,"alisema
Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alisema kitu pekee ambacho anaweza kukizungumza kwa uwakika ni kuwa Msuya alikuwa akisema ukweli hata kwenye mazingira yasiyofaa.
"Nimefanya nae kazi kwa muda mrefu zaidi, nimechota hekima zake kidogo, alikuwa ni jasiri na mtu ambaye anasema ukweli hata kwenye mazingira magumu ila alikuwa na maono ya mbali katika kuisimamia Amani, uadilifu na uchapaka kazi,
"Niongezee kidogo alichosema askofu Mono, pale kwa uuzaji wa kura, hili ni kwa watanzania wote na sio kwa wanamwanga tu, mtu yoyote anayetaka madaraka au aliopo madarakani apimwe kwa kazi aliyofanya na sio vinginevyo,"alisema Pinda.
Alisema watanzania wasikubali kuwa watumwa wa wataka madaraka na badala yake kujione mwenyewe kiongozi huyo ameacha alama gani au analeta tija gani na sio ametupa kiasi gani.
Akitoa salama za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu aliishukuru kamati ya maandalizi ya kitaifa kwa jitiada zao za kuhakisha mwili umefika salama katika mkoa wa Kilimanjaro na kuomba ushirikiano zaidi hadi kumpumzisha mzee Msuya.
"Maisha ya mzee wetu ni kitabu ambacho kimewafundisha wengi, matokeo ya kitabu hichi ni kujipima katika utekelezaji na kuitumikia jamii husika," alisema
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa