Mgombea Uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaomba radhi wananchi wa wilaya ya Same kwa kuchelewa kwa mradi wa maji ambao utakuwa suluhisho la tatizo la maji katika mji hou na maeneo ya jirani.
Akihutubia wananch katika mkutano wa kampeni ulifanyika katika uwanja wa soko la Kwasakwasa katika mji wa Same Mhe. Dkt. Magufuli amesema amesikitishwa sana na kucheleweshwa kwa mradi huo ambao utaanzia katika bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani Mwanga na kupita Same hadi Korogwe mkoani Tanga.
Aidha Mhe. Dkt. Magufuli amesema wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilion mia mbili ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2017 lakini hadi kufikia sasa umetekelezwa kwa asilimia sitini tu.
Katika kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika haraka iwezekanavyo Mhe. Dr. Magufuli amewaagiza Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akutane na mkandarasi ili ajue nini kilichokwamisha kukamilika kwa mradi huo na ampe taarifa kabla ya Mhe. Dkt. Magufuli hajamaliza ziara yake katika mkoa wa Kilimanjaro.
Mhe. Dkt. Magufuli ametumia fursa hiyo kutoa onyo kwa mkandarasi wa mradi huo kuacha kuzembea na kumpa muda wa siku thelathini kuona mabadiliko ili mradi huo kukamilika kwa wakati,
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa