• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kilimanjaro Region
Kilimanjaro Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kilimanjaro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia ya Mkoa
    • Viongozi wa Mkoa
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Sekretariati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
      • Trade and Investment
      • Administration and Human Resource Department
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Teknologia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ukaguzi wa Ndani
    • Miongozo
  • Wilaya
    • Hai
    • Moshi
    • Mwanga
    • Same
    • Rombo
    • Siha
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hai
    • Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
    • Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Same
    • Halmashauri ya Wilaya ya Siha
    • Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Uvuvi
  • Huduma Zetu
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Albam
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi kumsindikiza aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Cleopa David Msuya katika safari yake ya mwisho.

Posted on: May 13th, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na nje ya nchi kumsindikiza aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Cleopa David Msuya katika safari yake ya mwisho. 

Msuya aliyefariki Mei 7 mwaka huu katika hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam kutokana na ugonjwa na moyo ambapo ibada ya mazishi imefanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Usangi Kivindu na baadae kufuatiwa na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Kijiji cha  Chomvu kata ya Chomvu Usangi, wilayani Mwanga. 

Dkt. Samia alisema kuwa Mzee Msuya alikua zawadi si kwa familia tu  bali kwa Taifa zima ni mzalendo amekuwa mtetezi mzuri wa maendeleo ya Wanamwanga hivyo haishangazi kuona amepewa jina la Baba wa Mwanga.

Alisema kuwa, Msuya atakumbukwa kwa mambo mengi hasa kujitolea maisha yake yote kuwatumikia Watanzania katika nyazifa mbalimbali alizoshika aliweka rekodi mbili kubwa.

Alizitaja rekodi hizo kuwa ni Waziri aliyehudumu katika wadhifa wa Waziri wa fedha katika kipindi kirefu zaidi kwa nyakati tofauti 1972 hadi 1975, 1983-1985, 1985-1990, na pili  licha ya kuwa waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kipindi kifupi cha miezi 11 yeye ndio Mtanzania wa mwisho kushika nafasi hiyo kwani baada ya hapo tuliingia katika mfumo wa vyama vingi ambapo Makamu wa Rais alipatikana kupitia mgombea mwenza.

"Katika mengi yatakayokumbukwa nayo ni pamoja na mchango wake mkubwa wa kutafuta fedha kwa ajili ya kuunga mkono harakati za ukombozi kusini mwa Afrika akiwa Katibu Mkuu wa fedha mbali na kuangaika kutafuta fedha za matumizi ya serikali alikuwa na jukumu la kutenga bajeti kwa ajili ya harakati za ukombozi alisema Rais Dkt. Samia.

Mhe. Dkt. Samia alisema  kuwa, alikuwa miongoni mwa viongozi walioenda nchini China kwa ajili ya kutafuta fedha za mradi wa ujenzi wa reli ya Tazara uliosaidia sana harakati za ukombozi na ambao umeendelea kutunufaisha kiuchumi.

Aliendelea kudai kuwa, Msuya aliongoza mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi ili kuruhusu uchumi wa soko na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi hiki kilikuwa kipindi kigumu cha kukabiliana na upinzani na shinikizo kutoka kwa wafadhili wa kimataifa, wanasiasa nchini, wafanyabiashara wazawa na wasio wazawa na makundi mengine kazi yao wakiunga mkono mageuzi na wengine wakiyapinga kwa sababu zao binafsi.

"Wakati shilingi yetu inataka kushushwa thamani tulikuwepo wanaccm tulisukumwa kuandamana tukatoka maofisini kule Zanzibar mpaka CCM na kwa mara ya kwanza ndio niliimba jina Msuya kabla ya hapo nilikuwa nalisoma tu kwenye somo la siasa tulikuwa tunaimba Msuya usiruhusu shilingi yetu kushuka thamani" alisema Dkt. Samia.

Rais aliendelea kudai kuwa, Msuya amekumbana na mengi na pamoja na changamoto hizo nchi ilifanikiwa kuondosha shida kubwa zilizokuwa zinawakabili wananchi.

Alisema kuwa ili kujidhihirisha hilo, katika kitabu cha Rais Ali Hassan Mwinyi ametambua mchango wa Msuya katika mabadiliko ya kiuchumi kuelekea uchumi wa soko na amemshukuru sana kwa mchango wake kama Waziri wa fedha.

Mzee Msuya aliendelea kutoa michango kwa Taifa kupitia ushauri wake kwa viongozi mbalimbali waliopo Serikalini hata yeye mwenyewe alifaidika na kupata busara zake.

Aliongeza kuwa, kwa mara ya kwanza kumuona Mzee Msuya macho kwa macho ilikuwa mwaka 2015 mwezi Agosti wakati wa  kampeni ambapo yeye alipangwa kuanza na kanda ya Kaskazini mkoa wa Kilimanjaro ambapo alianzia Same na alipofika Mwanga alikuta mwanga hauwaki kabisa ni vurugu za waliokuwa wanawania Ubunge baina ya Jumanne Maghembe na Joseph Tadayo.


"Ilinibidi nipande huku juu kumfwata Mzee Msuya aje atupe maelekezo tufanye nini baada ya kupata ushauri wa Msuya nilishuka tena Mwanga ofisi za chama pale na kamati ya siasa tulipambana pale mpaka saa sita za usiku ndio tunapata muafaka tukaondoka hii ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana na Mzee Msuya" alisema Rais Samia 

Aliendelea kudai kuwa, katika vipindi vyote alivokutana na Msuya alikuwa na salamu mbili kubwa kwake la kwanza mradi wa maji Mwanga Same Korogwe na la pili ni barabara ya buy pass ya CD Msuya ambapo hiyo ndio iliyokuwa miradi miwili inayomkereketa na alitaka itekelezwe.

Alisema kuwa, mara ya mwisho alimuona mwaka huu katika uzinduzi wa mradi wa maji Mwanga Same alifika kushuhudia lile ambalo alitamani litokee.

Dkt. Samia alisema kuwa, alipopata taarifa ya kifo cha kiongozi huyo alisema Mungu asante ingekuwa mradi wa maji haukukamilika angemzika Mzee na moyo gani angejisikiaje lakini anakwenda kumzika lile tamanio la moyo wake likiwa limetimia.

Akizungumzia  Dkt Samia  alisema barabara ya CD Msuya buy pass tayari mchakato wake umeshaanza na awamu ya kwanza imeshatekelezwa ambapo madaraja kadhaa yamejengwa na kazi inaendelea wapo katika awamu ya pili.

Aliongeza kuwa, katika hadithi ya Msuya yapo mambo mengi ambayo viongozi waliopo wanapaswa kujifunza na kudai kuwa moja ya mafunzo hayo ambayo yataishi katika akili zao na yapo yatakayoishi kwenye mioyo na yapo yatakayoishi kwenye maisha.

Alisema kuwa, jambo la kwanza la kujifunza ni kuwa wapenda maendeleo na kutoacha kusimamia kile wanachokiamini bila kuyumbishwa na mtu yoyote na huyo ndio alikuwa Mzee Msuya.

Aliendelea kudai kuwa, kufanya kazi kwa uzalendo na uadilifu na uaminifu kama alivyokuwa Msuya aliamini katika matumizi mazuri na usimamizi wa karibu wa rasilimali za Taifa ili zilete tija kwa wananchi.

Jambo la tatu aliamini kwamba ujuzi na utaalam unanafasi kubwa katika kuleta maendeleo na hakuwa muoga katika mabadiliko. 

Akitoa mahubiri katika ibada hiyo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dkt. Alex Malasusa alisema kuwa, Msuya ni baba ambaye alitafuta kuwa na amani na watu wote. 

Dkt. Malasusa alisema kuwa, miongoni mwa watumishi wa Serikali waliokuwa makini ni Mzee Cleopa Msuya na watu walimheshimu sio kwa sababu alikuwa na nguvu ni kwa sababu ya hekima na busara zake.

"Hizi ndimi tulizonazo zinatukosesha sana Msuya alikuwa hata akikuonya unakubali maonyo yake kwa sababu unaona ni sawa sawa kwani alikuwa anatumia ndimi yake vizuri" Alisema Dkt. Malasusa. 

Na kuongeza "ushuhuda wa mzee Msuya unanishangaza sana viongozi wengi wa ngazi yake na hata wale wa ngazi ya chini wanamsifu kuitwa baba wa Mwanga sio kwa sababu ya uzee wake alikuwa sababu kubwa ya kuwafanya walio wengi watabasamu".


Aliongeza kuwa,wanyenyekevu ni wachache sana na marehemu Msuya ameonyesha unyenyekevu sio uoga wala sio uzembe ni kutafuta amani na kudai kuwa unyenyekevu ni ile hali ya kujishusha tayari kwa ajili ya kuwatumikia wengine ambapo Msuya haliliishi hilo. 

Alisema kuwa Msuya alipewa neema ya kusikiliza hata ulipokuwa unakwenda kwake alikuwa anakusikiliza kama hajui kumbe anajua sana. 

Askofu huyo alisema kuwa, anajua Rais anawategemea wastaafu kama Msuya kama washauri wake wa karibu sana na kudai kuwa huyu Mungu anayeaminiwa yeye moja ya sifa yake ni mshauri wa ajabu na ataendelea kumshauri Rais ili Taifa liendelee kusonga mbele. 

Pia aliwaambia wananchi wa Mwanga kuwa, walimuita Mzee Msuya kama baba wa Mwanga na kuwatia moyo kuwa Mungu ataendelea kuwa baba yao. 


SALAMU ZA FAMILIA. 

Akitoa salamu za Familia, Mtoto wa marehemu Msuya, Job Msuya alisema kuwa , Mzee cleopa Msuya aliomba familia yake kuhakikisha wanaikumbuka siku yake  ya kuzaliwa kwa kujenga chuo kikuu  cha kutumia elimu zaidi.

Hayo yamesemwa na mtoto wa marehemu, Dk John Msuya wakati akitoa neno la shukurani kwenye ibada maalumu ya mazishi ya Cleopa Msuya.

"Kwa hakika baba yetu hakupenda kufanyiwa sikukuu  yake  ya kuzaliwa lakini mwaka huu aliagiza afanyiwe na katika sikukuu hiyo ambayo ilikuwa ni January 4 mwaka huu,

Katika siku hiyo kulikuwa na mazungumzo mengi kwa wanamwanga waliouliza wafanye nini kumuenzi wapo waliosema   apewa jina la Barabara ya by pass iliyopo Mwanga.

Mtoto huyo aliendelea kudai kuwa, aliamua kumfuata Msuya na kumuuliza apewe nini ambapo alimjibu kuwa yeye lengo lake kujengwe chuo kikuu katika wilaya ya Mwanga. 

"Nikamuuliza chuo kikuu cha aina gani akasema sio vyuo ambavyo vinatumia vitabu vingi bali kitakachotumia ubongo cha technology na 'power Brain'. 

Pia alidai kuwa, alimsisitiza kuhakikisha Benki ya Mwanga hakika Benki aliyoianzisha haifi waitunze ili ijekuwa kubwa kama Benki nyingine zilizopo nchini. 


WASIFU WA MAREHEMU MSUYA. 

Cleopa David Msuya alizaliwa Januari 4 mwaka 1931 huko Shighatini Mwanga, na mwaka 1956-1961 alifanya kazi katika serikali ya Tanganyika kama Afisa Maendeleo ya jamii, na mwaka 1961 alipandishwa cheo kutokana na kazi yake nzuri hadi kufikia daraja la Naibu Kamishna maendeleo ya jamii wadhifa aliokuwa nao hadi mwaka 1964.

Kati ya mwaka 1964 na 1965 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya maendeleo ya jamii na Utamaduni wa Taifa, mwaka 1965 mpaka 1967 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makazi na Maendeleo ya Huduma za maji.

Mwaka 1967 na 1970 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya masuala ya uchumi na mipango ya maendeleo na mwaka 1970 mpaka 1972 alikuwa Katibu Mkuu Hazina na Wizara ya Fedha na Hazina. 

NYADHIFA KWENYE BUNGE NA BARAZA LA MAWAZIRI. 

Kati ya Februari 1972 na Novemba 1975 alikuwa Mbunge na Waziri wa Fedha, Novemba 1975 mpaka Novemba 1980 alikuwa Mbunge na Waziri wa viwanda. 

MBUNGE WA MWANGA NA WAZIRI MKUU. 

Novemba 1980 hadi Februari 1983 alikuwa Mbunge wa Jimbo la Mwanga na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Kati ya Februari 1983 na Novemba 1985 alikuwa Mbunge wa Mwanga na Waziri wa Fedha, mwezi Novemba 1985 mpaka Novemba 1990 alikuwa Mbunge wa Mwanga na Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Novemba 1990 mpaka Desemba 1994 alikuwa Mbunge wa Mwanga na Waziri wa Viwanda na Biashara. 


KUTEULIWA TENA NAFASI YA WAZIRI MKUU. 

Desemba 1994 aliteuliwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wadhifa aliokuwa nao hadi Novemba 1995 ambapo Novemba 1995 hadi Novemba 2000 alikuwa Mbunge wa Mwanga. 


NYADHIFA KWENYE CHAMA. 

Kati ya mwaka 1964 na 1977 alikuwa mwanachma wa chama cha Tanu ambacho kiliunga na chama cha ASP mwaka 1977 na kuzaliwa Chama cha Mapinduzi. 

Mwaka 1977 Msuya alikuwa mmoja wa wanachama waanzilishi wa ccm na mwaka 1982 hadi 1992 alikuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya ccm (Nec) na Kati ya 1992 na 1995 alikuwa Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya ccm. 

Mwaka 1995 jina la Cleopa David Msuya lilikuwa moja wapo ya majina matatu yaliyopitishwa na Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ili kupigiwa kura na Mkutano Mkuu wa CCM kwa nafasi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM. 

Mbali na waombolezaji kutoka Mwanga, viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali wakiwemo Makatibu wa kuu, Wabunge, Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Spika wa Bunge, Katibu Mkuu kiongozi, Mawaziri wakuu wastaafu pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya tano, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa walishiriki mazishi hayo.

Matangazo

  • Kwa Huduma Bora ya Ukumbi wa kisasa wa Mikutano, Tafadhali fika Ofisini au wasiliana nasi kwa S.L. P 3070, Moshi. au Piga simu namba 027 2758248/027 2751 February 03, 2020
  • ZOEZI LA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUANZA MEI 16 HADI MEI 22 2025 KILIMANJARO May 15, 2025
  • MRADI WA BOOST April 01, 2023
  • Angalia Zote

Habari

  • VIJANA NA WANAWAKE MSIKOPE BILA MALENGO

    May 15, 2025
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi kumsindikiza aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Cleopa David Msuya katika safari yake ya mwisho.

    May 13, 2025
  • Mwili wa Hayati Cleopa D. Msuya waagwa katika viwanja vya CD Msuya wilayani Mwanga

    May 12, 2025
  • SERIKALI KUTENGA BILIONI 7 KUTEKELEZA UJENZI WA BARABARA YA MABOGINI - KAHE

    May 04, 2025
  • Angalia Zote

Video

Kujisajili kwenye mfumo wa NeST - Hatua ya Awali
Video

Kiunganishi cha Haraka

  • Webmail
  • Malalamiko
  • Watumishi Portal

Tovuti zinazohusiana nasi

  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi (LIVE)
  • Mfumo wa Usambazaji Mafaili kwa njia ya Ki-Eletroniki (E-Office)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na Kufuatilia malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    17 Barabara ya Florida

    Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi

    Simu: +255 (027) 2754236/7

    Mobile:

    Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa