Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira ameahidi kushirikiana kwa karibu na jumumuiya za wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali wa mkoa wa Kilimanjarokatika kutatua kero zinazowakabili.
Mhe. Mghwira aliyasema hayo wakati akitoa hotuba ya kuahirisha kikao alichokiitisha kwa lengo la kukutana na wafanyabiashara ili kujadiliana kwa pamoja juu ya changamoto na fursa za kibiashara zilizopo mkoani Kilimanjaro.
Ameongeza kuwa serikali bado inautazama mkoa wa Kilimanjaro kama miongoni mwa mikoa muhimu katika kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla kwa kuzingatia fursa ulizonazo katika rasilimali watu yenye tabia ya kujituma katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.
Aidha Mhe. Mghwira amewahakikishia wafanyabiashara kuwa hoja zao zote walizoziwasilisha katika kujadili fursa na changamoto zitafanyiwa kazi kwa kuzingatia uwezo na mamlaka za maamuzi.
Alifafanua kuwa baadhi ya hoja na changamoto zilizowasilishwa zinaweza kushughulikiwa katika ngazi za mkoa na halmashauri na zingine hususan zinazohusu sera na miongozo ya kitaifa zitawasilishwa katika wizara zinashushughulikia sekta za fedha, kilimo, biashara na maji.
Kuhusu upatikanaji wa mitaji Mhe. Mghwira amesema bado taasisi za kifedha hazijajielekeza katika kutoa mikopo ya uwekezaji na baadala yake zimekuwa zikitoa mikopo ya kibiashara ambayo mkopaji huwekewa masharti ya kuanza kurudisha mikopo hiyo ndani ya muda mfupi.
Mhe Mghwira amezishauri taasisi hizo kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo inayotoa muda wa kutosha kwa wakopaji kujipanga na kuweza kurejesha mikopo wakiwa wameshaitumia kuwaingizia faida.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa