Wasimamizi na watoaji wa huduma ya elimu mkoani Kilimanjaro wametakiwa kutoa elimu ya maarifa itakayowasadia wanafunzi kuwa na uwezo wa kufanya kazi za mikono.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kwa wakuu wa shule na maafisa elimu kata wilayani Moshi Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira amewataka waalimu kuhakikisha kuwa elimu ya wanayoitoa kwa watoto isiwe ya darasani pekee bali watoe mafunzo ya vitendo ambayo yatahusu stadi za kazi.
Dkt. Mghwira amefafanua kuwa kumejengeka fikra hasi katika jamii kuwa kupinga ajira kwa watoto ni kutomfundisha mtoto kufanya kazi jambo ambalo amesema ni fikra potofu kabisa.
Ameongeza kuwa mtoto anaweza kupewa kazi kwa mujibu wa umri wake kama sehemu ya malezi ili awe na fikra za kujitegemea katika maisha yake.
Akitoa mfano wa shughuli za utunzaji wa mazingira Dkt. Mghwira amesema si makosa kumfundisha mtoto kupanda na kutunza miti ya matunda kwani faida ya kufanya hivyo ataiyona mapema akiwa shuleni kwa kunufaika kwa kivuli na matunda na hatimaye atakapomaliza masomo atakuwa ameshanufaika na elimu hiyo kwa vitendo.
Aidha Dkt. Mghwira ameongeza kuwa mawazo ya utoaji elimu ya kumjengea mtoto kuwa na fikra za kujitegemea yalianzishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kujenga taifa lenye watu wasio na fikra za utegemezi. " Wakati tulipokuwa watoto Mwalimu Nyerere alikuwa akituhimiza kuotesha chakula hata katika maeneo haya amboyo mnapanda mauau". Alifafanunua Dkt. Mghwira.
Awali akitoa taarifa ya mafunzo hayo kwa mkuu wa mkoa Katibu Tawala Msaidizi anayesimimaea elimu katika mko wa Kilimanjaro, Paulina Mkwama amesea kuwa mafunzo hayo yamehusisha washiriki 460 wakiwemo Maafisa elimu kata 168 na wakuuu wa shule 338 katika mkoa wa KIlimanjaro.
Mwalimu Mkwama alifafanua kuwa wamegawa washiriki katia makundi matatu yatakayopata mafunzo katika vituo vya Hai, Moshi na Same.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa