Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mgwira amefanya ziara kwenye gereza la karanga manispaa ya Moshi kukagua maendeleo ya kazi ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha kutengeneza viatu na bidhaa zingine zinazotokana na ngozi.
Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Mghwira alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa gereza la Karanga pamoja na kutembelea majengo mbalimbali yanayojengwa katika eneo hilo la mradi.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Karanga, Mkaguzi wa Magereza Rajab Igongi amesema kasi ya utekelezaji wa mradi huo imeongezeka zaidi kutokana kutatuliwa kwa changamoto zilizokuwa zikibili utekelezaji wa mradi huo.
Amezitaja changamo hizi kuwa ni pamoja na ufikishwaji wa fedha pamoja na mvua zilizokuwa zikinyesha na kupelekea kusuasua kwa ujenzi hapo awali.
Gereza la karanga kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF wanajenga kiwanda cha kutengeneza viatu pamoja na bidhaa zingine zitokanazo na ngozi kitakachogharimu shilingi za kitanzania bilioni 9.6.
Mkaguzi wa Magereza Igongi ameongeza kuwa wananchi wa mkoa wa kilimanjaro watanufaika kwa kupata ajira kwani kiwanda hicho kitaajiri wataalam mbalimbali ambao si askari kufanya kazi katika kiwanda hicho.
Adha Mkaguzi wa Magereza Igongi amessisitiza kuwa kiwanda hicho kitakapoanza kazi kitachangia mapato kwani ya nchi mamlakambalimbali za kusasanya mapato zitakusanya kodi kutokana na uzaisha wa kiwanda hicho.
Mradi huo ulianza mwezi Oktoba mwaka jana utarajiwa kukamilika itakapofika mwezi Machi mwaka huu. unatajiwa kukamilika.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa