Wadau wa maendeleo mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuendelea kujitokeza kutoa midsaada yao kwa wananchi waliopatwa na janga la mafuriko katika mkoa wa kilimanjaro.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mhe. dkt. Anna Mghwira baada ya kukabidhi misaada ya vyakula na mavazi uliotolewa na Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi.
Mhe. Dkt. Mghwira amelishukuru kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Moshi kwa kutoa gunia 12 za mahindi zenye jumla ya kg 1486 pamoja na mafurushi 15 vya nguo za watoto, wamama na wanaume.
Katika shukrani hizo Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema kwa niaba ya wanananchi na serikali mkoani Kilimanjaro anatambua na kuthamini msaada huo uliotolewa na kanisa katoliki jimbo la Moshi kuwataka wawkilishi wa Baba Askofu kufikisha salamu hizo za shukrani kwa Baba Askofu Ludovick Joseph Minde, askofu mkuu wa jimbo Katoliki Moshi.
Aidha Mhe. Dkt. Mghwira amesema ameridhishwa na namna Wakuu wa Wilaya walivyolishughulikia janaga la mafuriko katika wilaya zao.
Mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika yameathiri makazi na kuharibu vibaya mzao yaliyokuwa shambani katika wilaya za Moshi,Mwanga,Same na Hai.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa