Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu leo februari 25,2025 amefanya ziara Wilayani Mwanga kujionea maendeleo ya mradi mkubwa wa maji unaozunguka maeneo ya Same, Mwanga, na Korogwe. Ziara hii inakuja ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 9 Machi, 2025.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Babu alisema, "Mradi huu wa Maji ni matumaini makubwa kwa wananchi wa Same, Mwanga, na Korogwe. Huu ni mradi ambao umechukua muda mrefu, lakini kupitia juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameupatia mwarobaini wake kwa kutoa fedha nyingi na sasa mradi huu umefikia hatua nzuri na utakapozinduliwa utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi." Pia aliongeza kuwa mradi huu utaondoa changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji katika maeneo hayo na kuboresha huduma za kijamii.
Aidha, Mhe. Babu aliwataka wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro, hasa wa Wilaya za Same na Mwanga, kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan siku ya uzinduzi wa mradi huo, na kumshukuru kwa kutoa kipaumbele kwa masuala ya miundombinu muhimu ya maji.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa