Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amewataka Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Meya, Wakuu wa Wilaya zote sita kuhakikisha barabara zote zisizo chini ya TARURA na TANROADS kuhakikisha zinafanyiwa marekebisho na kupitika muda wote katika mwaka.
Ameyasema hayo Disemba 13,2024 katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambapo alisema barabara zote lazima zijengwe na kukarabatiwa kurahisisha mambo ya kiuchumi.
Amesema "Niwaagize na kuwasisitiza Wakurugenzi wa Malaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa huo na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali katika wilaya, barabara zote ambazo hazihudumiwi na wakala wa barabara TANROADS na TARURA ni wajibu wao kuzifanyia marekebisho na kuweka taa za barabarani kwani huchangia asilimia kumi ya pato, "
Amesema lengo kuu la Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha kuwa miundombinu ya Barabara inakuwa rafiki yaani zinapitika majira yote na hivyo kuwawezesha wananchi kufika kwa wakati maeneo yote na kujiongezea kipato katika shughuli za kiuchumi.
Amesema licha ya Serikali kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ukarabati wa barabara, kumekuwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu kama vile uvamizi wa hifadhi ya barabara, wizi na uharibifu wa taa za barabarani kinyume na sheria za barabara.
"Kumekuwa na ucheleweshaji wa kuchukuwa hatua za kisheria , hivyo naelekeza kuwa Wakuu wa Wilaya , Meya, Wenyeviti wa Halmashauri na Mamlaka za Kisheria wakishirikiana na TANROADS na TARURA kulinda miundombinu na watakaokaidi wachukuliwe hatua mara moja,"amesema Babu.
Amesema Mkoa utaendelea na utaratibu wa kufanya ukaguzi wa matengenezo ya barabara lengo ni kuhakikisha barabara zote zimejengwa katika viwango vilivyokabaliwa.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa Kilimanjaro, Yusufu Nzowa alisema barabara ni moyo wa uchumi hapa nchini hivyo ni wajibu wa kila aliyepewa dhamana kuhakikisha anatekeleza wajibu wake.
Amesema watakuwa wakali kwa wakandarasi wazembe, wanaofanya kazi chini ya kiwango na wanaochelewesha kazi hizo.
"Wananchi wetu wanategemea barabara hizi katika kufanya shughuli za kiuchumi, huu ni moyo wa Uchumi wetu. Tunataka kazi zinazofanyika zionyeshe thamani ya pesa zinazotolewa,"Amesema Nzowa.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa