Mkuu wa Mkoa wa KilimanjaroMhde. Dkt. Anna Mghwira amezitaka taasisi za serikali zinazosimamia miundombinu ya barabara na maji ya mvua kushirikiana ili kuhakikisha mafuriko yanayosababishwa na mapungufu ya miundombinu hayatokei tena na kudhuru wananchi.
Dkt. Mghwira ameyasema hayo wakati wa kutoa shukrani kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambayo imetoa jumla ya tani kumi za unga wa mahindi kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika .
Mhe. Dkt. Mghwira amefafanua kuwa sehemu kubwa ya mafuriko yamesababishwa na mapungufu ya miundombinu iliyotakiwa kuelekeza maji ya mvua miton, mabwani na kwenye mifumo rasmi ya umwagiliaji, hivyo basi amesisitiza kuwepo kwa mawasiliano ya karibu kati Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADs) na Taasisi ya Umwagiliaji ili kufanya kazi kwa kushirikiana na kuhakikisha tatizo halijirudii tena.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kutoa salamu za shukrani kwa TBL , Katibu Tawala wa Mkoa wa kilimanjaro Dkt. Khatib Kazungu amesema mifuko hiyo ya unga wa mahindi itagawiwa kwa halmashauri zilizopatwa na janga la mafuriko kwa kuzingatia ukubwa wa athari za mafuriko hayo kwa kila halmashauri.
Dkt. Kazunguzungu amewasilisha mchanganuo wa mgao huoa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ipata mifuko 67, Halmashauri ya wilaya ya Moshi itapata mifuko 55 , Manispaa ya Moshi itapata mifuko 29 na Halmashauri ya Wilaya ya Same itapata mifuko 250.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa