Wafanyabiashara na taasisi mbalimbali za kijamii zimehamasishwa kuunga mkono kampeni ya “Kili Challenge” inayoendeshwa na mgodi wa dhahabu wa geita kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya UKIMWI.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira alipokuwa akiwapokea Wapanda Mlima Kilimanjaro na Waendesha Baiskeli waliofadhiliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya UKIMWI.
Mhe. Mgwira amesema ushiriki wa wadau wengi zaidi utasaidia kuwa na uwezo wa kufikia malengo ya kitaifa ya kuwa na sifuri tatu ambazo ni kutokuwa na maambukizi mapya, unyanyapaa na kutokuwa na vifo vitokanavyo na UKIMWI.
Aidha Mhe. Mghwira ameushukuru Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) pamoja na wadau washiriki, katika kuandaa na kuwezesha kampeni ya ’’kilimanjaro HIV and AIDS challenge” kila mwaka.
Mgodi wa Dhahabu wa Geita umekuwa ukiendesha kampeni inayoitwa ’’kilimanjaro HIV and AIDS challenge” ambapo kila mwaka hufadhili wapanda mlima Kilimanjro ili kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya UKIMWI.
Kwa mwaka huu jumla ya wapanda mlima 50 waliopanda kupitia lango la machame na kushuka kupitia lango la Mweka lilipo Kibosho wilayani Moshi huku waendesha baiskeli 37 waliendesha baiskeli kuuzunguka mlima Kilimanjaro.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa