Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Nurdin H. Babu, leo amepokea ugeni kutoka kwa Bw. Noud Van Hout, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Shirika la Watoto Foundation, pamoja na Dkt. Andrea R. Modest, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo lenye makao makuu yake Usa River, Arusha.
Kufuatia ziara hiyo, Bw. Van Hout alieleza kuwa lengo la ujio wao ni kujitambulisha rasmi katika Mkoa wa Kilimanjaro na kueleza mikakati yao ya kupanua huduma za shirika hilo katika mkoa huo. Watoto Foundation inajikita katika kusaidia watoto wa mitaani wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwajengea uwezo na kuwapa fursa za maisha bora.
Aidha, Rc.Babu ameahidi mkoa wake utatoa ushirikiano ili kufanikisha malengo ya shirika hilo,huku akiwataka a kuzingatia sheria, kanuni, miongozo, na taratibu za nchi ili kuhakikisha huduma wanazotoa zinazingatia misingi inayostahili.
Kupitia ushirikiano huu, Shirika la Watoto Foundation linatarajiwa kusaidia kupunguza idadi ya watoto wa mitaani katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwawezesha kupata elimu, mafunzo ya stadi za maisha, na msaada unaohitajika kwa ajili ya ustawi wao.
17 Barabara ya Florida
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: +255 (027) 2754236/7
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz / ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa