Wananchi wa wilaya ya same wametakiwa kuchukua hatua za makusudi ili kuhakikisha wanalirejesha zao la kahawa ambalo kwa sasa wakulima wengi wameacha kulima kutokana na changamoto mbalimbali.
Akiongea na wananchi wa kijiji cha Vudee kata ya Vudee wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjarao, Mhe. Anna Mghwira amemuagiza afisa tarafa na mtendaji wa kata kutoa taarifa muhimu za zao hilo ikiwa ni pamoja na idadi ya mashamba yanayolima kahawa, idadi ya wakulima na mahitaji ya miche ya kisasa ya kahawa.
Mbali na hilo Mhe. Dkt. Mghwira amewataka wataalam wa kilimo wilayani same kufanya utafiti kujua wakulima wa kahawa wanahitaji elimu gani ili waandaliwe mafunzo yatakayowawezesha kufanya shughuli zao kwa mafanikio zaidi.
Mhe. Mghwira amesema wanachi wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo kwani nchi nyingi duniani zimethibitisha kuwa kahawa ya Tanzania ni kahawa bora na inafanya vizuri kwenye soko la dunia.
Aidha Mhe. Mghwira amewaponngeza wananchi wa Vudee kwa kuendeleza kilimo cha matuta ambacho ni muhimu kwa kuhifadhi rutuba na unyevu kwenye mashamba.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa