Serikali mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kurejesha mali zenye thamani zaidiya shlingi bilioni mbili ziizokuwa zimeuzwa na chamakikuu cha ushirikamkoani Kilimanjaro kinyume na sheria na taratibu za ushirika.
Akizungumza na waandishishi wa habari,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt.Anna E. Mghwira amesema mali zilizorejeshwa ni pamoja na viwanja vitano vilivyopo maeneo ya Msaranga ambavyo kwa sasa ni makazi ya watu, maghala matano yaliyopo maeneo ya viwandani, jengo moja kubwapamoja na eneo lenye mchanganyiko wa majengo ambalozamani lilikuwa hoteli ya ushirika.
Aidha amefafanua kuwa watu walionunua mali hizo ambao miongoni mwao wamo wafanya biashara na wananchi wengine wanaofanya shughuli mbalimbali wametakiwa kuzirejesha mali hizo au kutoa fedha zenye thamani ya mali endapo kwa sasa haimiliki mali hiyo.
Mbali hayo, Mhe. Dkt. Mghira ametumia fursa hiyo kutoa taarifa ya kikao kitakachofanyika siku ya Ijumaa ya taerehe 13, Septemba 2020 kitahusisha viongozi wa tasisi za umma, wafanya biashara na wananchi walio nunua mali za ushirika kinyume na sheria kwalengo la kuwasidia kujua sheria na taratibu zinazohusika ili kuepuka kutoingia kwenye mazingira tatanishi wanapotaka kununua mali zinazomilikiwa na ushirika.
Kuhusu taratibu za kisheria Mhe. Dkt. Mghwirs amesma watu wote waliohusika kuuza mali hizo watachukuliwa hatua za sheria ikiwa ni pamja na kufikishwa mahakamani.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa