Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Dkt Anna Mgwhira ameupongeza uwongozi wa kiwanda cha Sukari TPC kwa kuanza uzalishaji wa Sukari katika msimu wa 2020/2021ambapo wanatarajia kuzalisha takribani tani elfu 93 za sukari licha ya kukabiliwa na changamoto ya mafuriko ambayo imeathiri uzalishaji wa miwa katika mashamba kiwanda hicho
Akizungumza katika ghafla ya uzinduzi wa msimu huo Dkt. Mgwhira amesema hatua hiyo itasaidia kuwaondolea adha walaji kulanguliwa kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kuagiza sukari kutoka nje ya nchi na kuiuza kwa wananchi kwa bei ghali.
Aidha Dkt.Mgwhira amewataka wafanyabiashara kuwa waadilifu kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazotolewa na bodi ya Sukari ikiwemo ukomo wa bei elekezi ifikapo juni 30/ 2020 kwani kuanzia kipindi hizo sukari itakayozalishwa ndani ya nchi itatosha kukidhi mahitaji ya wananchi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Utawala wa kiwanda cha TPC Bw. Jaffary Ally amesema uzalishaji wa sukari umeshaanza rasmi ambapo wanatarajia kuzalisha kwa ziada ikilinganishwa na msimu uliopita kwa kuzalisha takribani tani 93,000 kutoka tani 89,000 walizozalisha msimu uliopita ili kutatua changamoto ya uhaba wa sukari hapa nchini.
Bw. Ally amesebainisha changamoto kubwa waliyonayo kwa Sasa ni mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika ambapo maji yamefurika mashambani na kuharibu miwa iliyokuwa shamabani pamoja na miundombinu ikiwemo na barabara na reli zinazotumika kusafirisha miwa kutoka mashambani hadi kiwandani .
Aidha Bw. Ally amewataka wasambazaji wa Sukari kufuata taratibu za usajili zinazotolewa na Serikali kupitia Bodi ya Sukari ikiwemo kutofungasha sukari kwenye mifuko yenye ujazo wowote ambayo haina nembo ya mzalishaji kwani ni kinyume cha sheria na kunahatarisha afya za walaji.
Florida Street
Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi
Simu: 027 2758248/027 2751
Mobile:
Anuani pepe: ras@kilimanjaro.go.tz/ras.kilimanjaro@tamisemi.go.tz
Hakiimiliki©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Haki zote zimehifadhiwa